Kundi la Hezbollah limedai “ushindi” dhidi ya Israel baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema wapiganaji wake wako tayari kukabiliana na vitisho vya Israel siku zijazo
Kundi la Hezbollah limedai “ushindi” dhidi ya Israel baada ya kusainiwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, likisema wapiganaji wake wako tayari kukabiliana na vitisho vya Israel siku zijazo.
Licha ya vikosi vya Israel kusababisha hasara kubwa kwa kundi hilo, ikiwwemo kuuawa kwa kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah, limesema Israel ilishindwa kukalia miji yoyte au kuunda eneo la usalama.
Mkataba wa kusitisha mapigano unaitaka Hezbollah kuondoka kaskazini mwa Mto Litani na kuvunja miundombinu yake ya kijeshi kusini mwa Lebanon.
Hezbollah pia ilidai kufanya zaidi ya operesheni 4,637 za kijeshi dhidi ya Israel tangu Oktoba 2023 na kuahidi kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina.