Michezo

Maneno ya Rais wa Simba baada ya hizi droo zao ligi kuu

on

soccerRais Simba Evans Aveva kwa mara ya kwanza amefungua mdomo wake na kulizungumzia suala la sare mbili katika mechi zao za Ligi kuu bara ambapo Rais huyu amewataka mashabiki na wanachama wa Simba kuungana na kuwa pamoja katika kipindi ambacho alikiita hawajapoteza wala kufanya vizuri.

Baada ya hayo akasema anamuamini Kocha Patrick Phiri hivyo wampe muda kidogo kwa kuwa wanapita kwenye kipindi cha mpito >>>  “Hatujafanya vibaya wala kufanya vizuri, sare mbili na hakuna mchezo tuliopoteza, ni suala la kujipanga ili kuangalia tutafanya nini katika mechi zinazofuatia, uongozi una changamoto nyingi utaona tulifanya kila linalowezekana kwenye uchaguzi baadaye kwenye usajili lakini sasa bado mambo hayajakaa vizuri, ni suala la kupambana tu

Tupia Comments