Michezo

Baada ya ofa ya kwanza kupigwa chini, Man City watuma nyingine kumpata Sterling 

on

  Zikiwa zimebaki siku takribani 18 kabla ya dirisha la usajili barani ulaya halijafunguliwa rasmi.

 Klabu ya Manchester City baada ya kuporwa ubingwa wa England sasa imeanza kujipanga upya ili kurudisha himayani ubingwa huo na makombe mengine.

Siku ya jana klabu hiyo ilituma ofa rasmi ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Raheem Sterling, lakini Liverpool waliikata ofa ya kwanza ya paundi millioni 30.

Saa 24 baada ya jaribio lao kukwama, Man City wanaripotiwa kutuma ofa nyingine ambayo itakaribia kiasi cha £50m wanayoitaka Liverpool ili kumuuza mchezaji huyo.

Wakati huo huo City wanaripotiwa kujiandaa kutuma ofa ya paundi millioni 58 kwa Juventus ili kupata saini ya mchezaji Paul Pogba.

Tupia Comments