Michezo

Baada ya Schweinsteiger – Man United yakamilisha usajili wa kiungo huyu

on

Masaa kadhaa baada ya klabu ya Manchester United kukamilisha usajili wa beki wa kimataifa wa Italia Matteo Darmian na kiungo Bastian Schweinsteiger kutoka Bayern Munich, leo hii klabu hiyo imetangaza kuafikiana makubaliano na Southampton juu ya usajili wa kiungo Morgan Schnederlin.

  
Man United na Southampton wamekuwa na mazungumzo kwa muda wa wiki kadhaa sasa na hatimaye vilabu hivyo usiku wa kuamkia leo vilikubaliana bei ya uhamisho ya £25m kwa ajili ya Schnederlin.

Southampton walithibitisha kuikataa ofa ya kwanza ya Man United mapema wiki iliyopita, lakini yakiwa yamebaki masaa kadhaa kabla ya United kwenda kwenye Tour, hatimaye klabu hiyo imekubali ofa ya United.

   Schneiderlin aliyejiunga na Southampton mwaka 2008 akitokea Strasbourg kwa ada ya uhamisho wa £1.2m – jana usiku alifanyiwa vipimo vya afya na United na leo hii kabla ya safari wanategemea kutambulishwa rasmi yeye na mwenzie Bastian Schweinsteiger.

Tupia Comments