Baada ya wananchi zaidi ya mia mbili kuaandamana na kufunga barabara kwa zaidi ya Saa sita kwa madai ya ukosefu wa maji katika kijiji cha Losintai katika kata ya Oljoro namba tano Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Waziri wa Maji Juma Aweso ameingilia jambo hilo nakulitilia mkazo nakusema kuwa mpango huo unatakiwa kukamilika ndani ya mwezi mmoja wananchi waanze kupata maji
Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Mkoa wa Manyara amesema mradi wa upatikani wa maji ulikuwa kwenye mpango na ulikuwa ushaanza kutekelezwa na leo Waziri wa Maji Juma Aweso amempigia simu na ametaka maji yapatikane September 30,2024
“Mheshimiwa Mkuu wa wilaya mpango uliopo katika kijiji cha Lesinyai unafahamika,baada ya tukio la jana sisi tuna mifumo yetu ya kutoa taarifa za miradi,Viongozi wangu akiwemo Waziri wa Maji alinipigia na akaridhia mpango huu ukamilike September watu wapate maji”-Mhandisi Wolter Kirita Meneja RUWASA
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Fack Lulandala alikutana na wananchi kwemye Mkutano wa Hadhara nakuzungumza nao
Mambo mbalimbali na aliwaagiza polisi kutokutumia bomu hata moja kwa wananchi