Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limesema linamtafuta mkazi wa Kata ya Magugu wilayani Babati, Frednand Yohana ambaye anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 11.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Benjamin Kuzaga ameyasema hayo Jumatatu Desemba 13, 2021 mjini Babati wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Kamanda Kuzaga amesema mkazi huyo wa Magugu alikuwa anambaka mtoto wake wa kike mwenye umri wa miaka 11 (jina lake linahifadhiwa) usiku wakati mke wake na watoto wengine wakiwa wamelala.