Habari za Mastaa

Mchekeshaji Baba Levo nae kaingia kwenye Siasa au ndio zile fix zake?

on

BABA LEVO

Huu ndio mwaka 2015, mwaka wa Uchaguzi TZ, headlines za siasa ziko na sisi mara zote… Tulizoea kumsikia kwenye #Amplifaya kwenye zile @FixzaBabalevo akipiga story na watu wake mtaani, utani wake kwa wasanii na mastaa wa TZ.. Jamaa ndio kusema kaamua kuwafuata akina Afande Sele, Prof. Jay na Wema Sepetu kwenye Siasa? 

Baba Levo alionekana kwenye Stage Kigoma yeye pamoja na Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe.. kuna kingine kiliendelea huko?

Post ambayo imewekwa kwenya ukurasa wa CloudsFM on @Instagram imeandikwa hivi >>> “Baada ya @wemasepetu – sasa ni zamu ya @babalevo !! Msanii huyo kutoka Kigoma, ambaye ni mwanachama wa chama cha ACT kinachoongozwa na @zittokabwe, ametangaza kwamba anatarajia kugombea Udiwani Kata ya Mwanga Kaskazini – KIGOMA!!! Kila kheri Baba Levo!!” >>> @cloudsfmtz

Namtafuta Baba Levo, tutayasikia mengine Exclusive kuhusu yeye na safari yake kwenye Udiwani, kaa karibu na #Amplifaya pamoja na millardayo.com kwa ajili ya kuupata mwendelezo wa hii story mtu wangu.

Tupia Comments