Mtangazaji wa Clouds Media na Mwenyekiti Tasisi ya “Babuu Cancer Foundation” Sedou Mandingo maarufu “Babuu wa kitaa” ameandaa matembezi ya furaha yatakayofanyika December 28 2024 Jijini Mwanza yakilenga kutoa elimu ya Saratani.
Babuu akiwa ameongozana na Wataalamu wa Afya, amezungumza na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, ameeleza kuwa Kampeni yake ya ‘Happy Walk’ ina lenga kutoa elimu zaidi kuhusu ugonjwa wa Saratani kuifahamisha jamii kwamba Saratani inatibika.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Matibabu Babuu Cancer Foundation Dkt. Frank Rutachunzibwa amesema hali ya ufahamu kuhusu saratani kwa Kanda ya Ziwa inaongezeka kutokana jamii kuwa na mwamko wa kujitokeza mapema Hospitali kufanya uchunguzi wa hiari.
Ameongeza kwa kuwaomba wakazi wa Mwanza kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Nyamagana kuanzia saa 12 asubuhi kushiriki matembezi hayo ya furaha yatakayopambwa na Burudani mbalimba