Michezo

Babu wa miaka 74 aandika rekodi, mchezaji mkubwa duniani

on

Mchezaji Ezzeldin Bahader ,74, raia wa Misri sasa ni wazi ameingia katika rekodi ya vitabu vya dunia (Guinness World Records) ya kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi duniani  kucheza soka.

Ezzeldin Bahader sasa anatambulika rasmi na Guinness kuwa mchezaji soka mwenye umri mkubwa zaidi katika level ya professional akiwa na miaka 74.

Rekodi hiyo Ezzeldin Bahader ameiweka baada ya kucheza dhidi ya El Ayat katika mchezo wa daraja la tatu nchini Misri na kupoteza kwa magoli 3-2.

Ezzeldin Bahader alikuwa aweke rekodi hiyo toka mwezi March lakini mlipuko wa virusi vya Corona vikamkwamisha kutokana na kushindwa kucheza mechi yake ya pili ya mechi rasmi za mashindano kama alivyotakiwa na Guinness.

Bahader ni baba wa watoto wanne na babu wa wajukuu sita, alicheza mechi hizo kwa ajili ya kuandika rekodi,  mechi ya kwanza alicheza March 7, mzee huyo November 3 2020 anatimiza miaka 75.

Soma na hizi

Tupia Comments