Leo December 28 2024, Mtangazaji wa Clouds Media Sedou Mandingo maarufu Babuu wa Kitaa (@babuuwakitaa_tz) na Tasisi yake ya ‘Babuu Cancer Foundation’ kupitia Kampeni yao ya Saratani, wamefanikiwa kufanya matembezi ya furaha (Happy Walk) katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Mwanza.
Matembezi hayo yameongozwa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi, Wabunge Stanislaus Mabula na Angelina Mabula pamoja Wakazi wa Jiji la Mwanza.
Mkoa wa Mwanza unakuwa ni mkoa wa pili kufanyika kwa Kampeni hii baada ya Mkoa wa Tanga, ikilenga kutoa elimu ya Saratini na kuwakumbusha wananchi kwenda kufanya vipimo kwa kuwa Saratani inatibika na vipimo ni bure.
Kampeni ya ‘Happy Walk’ inabebwa na kauli mbiu inayosema Kitaa ni muhimu kufahamu mafanikio katika Sekta ya Afya.