Mtangazaji wa clouds Fm na clouds Tv Sedou Mandingo maarufu kwa jina la Babuu wa kitaa kupitia taasisi yake ya Babuu cancer foundation siku ya leo ametambulisha kampeini yake mpya ambayo inajulikana kama Saratani kitaa huku ikiwa na kauli mbiu ya “kitaa ni muhimu kufaham mafanikio sekta ya afya” ambayo itaanzia jijini mwanza huku ikiwa na malengo ya kuzunguka mikoa yote Tanzania
Akizungumza na wanahabari Babuu wa kitaa amesema kuwa kampeni yake hii ina malengo ya kutoa elimu kuhusu saratani kwa watu mbali mbali hasa mtaani huko huku ikiwaelezea ni namna gani wanaweza kupata vipimo au hata matibabu kupitia hospitali zetu za ndani ambazo tayari zimeboreshwa na vifaa vya kisasa vimeletwa Aidha Babuu amesema ataongozana na wasanii mbali mbali katika kutoa elimu hiyo
Itakumbukwa babuu wa kitaa ni muhanga wa saratani ambaye aliumwa kwa muda mrefu na kubahatika kupata matibabu na kupona kabisa na ndio akaamua kuanzisha Babuu cancer foundation.