Jamii nyingi kila moja imekua na imani tofauti juu ya jambo fulani lakini baadhi ya imani hizo hufanana kutokana na tukio husika.
Hii tunaweza kuita moja ya tukio la unyanyasaji kwa mtoto, baada ya mama mmoja Rakesh Kumar, ambaye ni mganga wa kienyeji huko India kumlazimisha mtoto wa siku mbili kutembea akiamini atapona.
Mtoto huyo alikuwa akisumbuliwa na homa kali na wazazi wake kuamua kumpeleka kwa mganga huyo ambaye alimchukua na kumlazimisha kutembea akiwa uchi huku akiwa amemkaba koo.
Pamoja na watu wengi kushuhudia tukio hilo hakuna aliyetokea kumsadia mtoto huyo ambaye alikuwa akilia sana baada ya kulazimishwa kutembea.
Baada ya tukio hilo mama mzazi pamoja na mganga huyo walifunguliwa mashtaka huku mtoto huyo akipelekwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
https://www.youtube.com/watch?v=mawvFgA8q_A
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.