Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

Rapper T.I atajwa kwenye list ya watu watakaosaidia jela ya Atlanta

on

Kwa nujibu wa mtandao wa US News umeripoti kuwa rapper T.I ni miongoni mwa watu walioteuliwa kwenye masuala ya kuisaidia jamii hasa kwenye masuala ya haki za wafungwa na magereza ya Atlanta nchini Marekani.

Inaelezwa kuwa mji huo umeteua jumla ya watu 25 ambapo inaripotiwa kuwa T.I amekuwa akijishughulisha na masuala ya kupigani haki za makosa ya jinai kwenye mji huo wa Atlanta huku jukumu kubwa la watu walioteuliwa ni kuzisaidia jela za mji huo ambazo uhifadhi watu wanaovunja sheria ndogo ndogo za kanuni za Atlanta.

Inatajwa kuwa kikao cha kwanza kwa ajili ya kushauriana vitu vya kufanya kitafanyika July 16,2019 na mapendekezo watakayokua nayo yatafikishwa kwa Meya wa mji huo Bi Keisha Lance  ambapo yatapitiwa na kupitishwa. 

VIDEO: ULIPITWA NA HII YA SIKU 7 GEREZANI, WEMA SEPETU AKIRI KUPITIA WAKATI MGUMU? BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA 

Soma na hizi

Tupia Comments