Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

P Diddy akutana na familia ya Lori Harvey (+Picha)

on

Baada ya kuwa na tetesi kuwa rapper P Diddy yuko kwenye mahusiano mapya na mwanadada Lori Harvey ambaye aliwahi kuwa mapenzini na Justin Combs ambaye ni mtoto wa P Diddy sasa penzi lao linazidi kushamiri.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umezinasa picha za rapper huyo akiwa na mpenzi wake Lori  pamoja na wazazi wa mwanadada huyo ambaye ni mtangazaji maarufu nchini Marekani Steve Harvey na imedaiwa kuwa Diddy pamoja na familia ya mpenzi wake wapo nchini Italy kwa ajili ya mapumziko.

Kwa mujibu wa mtandao wa Rap Up uliwahi kuripoti kuwa mwanadada huyo aliwahi kuvalishwa pete ya uchumba na Diddy kitu ambacho hakijathibitishwa mpaka leo na imeripotiwa kuwa penzi kati ya Justin Combs na Lori lilivunjika.

VIDEO: NANDY KATOA YA MOYONI KWA MSANII ANAYEMSEMA VIBAYA ‘ANA WIVU HATUENDANI’

Soma na hizi

Tupia Comments