Habari za Mastaa

Achana na ngoma ya ‘Blow My Mind’ Davido kuileta nyingine na Chris Brown

on

Baada ya mkali kutokea Nigeria Davido kuidondosha kolabo ya ‘Blow My Mind’ na mkali wa miondoko ya RnB Chris Brown siku ya June 30,2019 katika mtandao wa You Tube ikiwa mpaka sasa wimbo huo umetazamwa na watu zaidi ya Mil. 8 inaelezwa kuwa hiyo inaweza ikawa ni trailer tu.

Inaripotiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kolabo kibao kuachiwa mbeleni hii ni baada ya Davido kupost kupitia insta story yake akiwa kwenye video call na Chris Brown na kuandika ‘Another One’ akimaanisha nyingine.

Mpaka sasa inaripotiwa kuwa Davido ameshaingia studio na kufanya ngoma mpya na wakali kutokea Marekani akiwemo mwimbaji/mwigizaji Ludacris, mtoto wa Diddy (King Combs) na mtayarishaji wa muziki Timberland.

VIDEO: FID Q AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WAKATI WA UZINDUZI WA ALBUM YAKE, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA MWANZO MWISHO

Soma na hizi

Tupia Comments