Habari za Mastaa

Taylor Swift aongoza List ya Mastaa walioingiza pesa nyingi 2019

on

Kwa mujibu wa jarida la Forbes limetaja list ya watu maarufu duniani waliopo kwenye uwanja wa burudani, michezo n.k wanaoingiza pesa nyingi (The World’s Highest Paid Celebrities) ikiwa list hiyo imeongozwa na mwimbaji Taylor Swift.

Mwimbaji Taylor Swift amemtupa mbali Kylie Jenner na kutajwa kuwa ameingiza pesa nyingi kwa mwaka huu tokea June 2018- June 2019 akiwa ameingiza kiasi cha zaidi ya shilingi Bilioni 400 za Kitanzania huku ikielezwa kuwa ametengeneza pesa nyingi kupitia ziara yake ya muziki ‘Reputation Stadium Tour”.

Ziara ya muziki aliyoifanya Taylor Swift iliyoanza May 2018 mpaka November 2018 imetaja kumuingizia kiasi cha pesa zaidi ya shilingi Bilioni 700 za Kitanzania kwa ujumla ikijumuisha na mikataba ya kampuni alizokuwa akifanya nazo kazi ikiwemo Apple, AT&T.

FULL LIST HII HAPA-:

10.Canelo Alvarez (Bondia)

9.Dr. Phil MGraw (Mwandishi wa vitabu)

8.The Eagles (Rock Band)

7. Neymar (Mcheza Mpira)

6.Cristiano Ronaldo (Mcheza Mpira)

5.Ed Sheeran (Mwanamuziki)

4.Lionel Mess (Mcheza Mpira)

3.Kanye West (Rapper)

2.Kylie Jenner (Mfanyabiashara)

1.Taylor Swift (Mwimbaji)

VIDEO: IRENE UWOYA NA BATULI WAIZUNGUMZIA SWAHILIFLIX, MTANDAO UTAKAOUZA KAZI ZAO

Soma na hizi

Tupia Comments