Habari za Mastaa

Jose Chameleon na Bob Wine waungana kufanya Siasa

on

Inaripotiwa kuwa mwimbaji na Mbunge Bob Wine alikutana na Jose Chameleon Jumapili ya July 14,2019 na walizungumza kuhusu harakati za siasa nchini Uganda na kuelezwa kuwa waliafikiana kuungana pamoja ili kuleta mabadiliko nchini humo.

Jose Chameleone ambaye kwa sasa amejikita kwenye masuala ya siasa alikiri kuwa amehamasishwa na rafiki yake Bob Wine kuingia huko lakini kwa upande wake atagombea nafasi tofauti. Bobi Wine ambaye alikamatwa mara kadhaa kutokana na kupinga vikali utawala wa Rais Yoweri Museveni anatazamiwa kugombea kiti cha Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2021. 

“Rafiki yangu Jose Chameleon alinitembelea na tuliongea kuhusu yanayotarajiwa nchini na marengo yake kwenye siasa, aliniambia mawazo yake kuungana na People Power nilimshauri kuwa anayo nafasi ya kuwaamisha kundi la wanyanyasaji kuwa atasimama nao” >>>aliandika Bobi Wine.

VIDEO: KAFUNGUKA “NIKO NA MPENZI, NAKULA BATA, NINA NYUMBA MBEZI BEACH”

Soma na hizi

Tupia Comments