Habari za Mastaa

Mwanasheria wa 21 Savage aongezeka katika kesi ya Rapper Tekashi

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa Rapper Tekashi 69 ambaye bado anasota gerezani ameamua kuongeza Mwanasheria mwingine kwa ajili ya kuendesha kesi yake inayomkabili ya kujihusisha na mpango wa vurugu na kumiliki silaha.

Imeelezwa kuwa siku ya Jumanne July 9,2019 kutokana na nyaraka za mahakama zimeripoti kuwa  mwanasheria Alex Spiro ambaye Jay-Z alimchagua kusimamia kesi ya Rapper 21 Savage ndiye ameongezeka kwenye orodha ya wanasheria ambao watamsimamia Tekashi kwenye kesi yake inayomkabili.

Inadaiwa kuwa Tekashi atapandishwa kizimbani kusikiliza kesi yake September 4,2019 ambapo tokea November 18,2018 alikua akishikiliwa na kusota kwenye jela ya kijasusi nchini Marekani.

AUDIO: VERA SIDIKA KAJIBADILISHA RANGI, ERIC OMONDI ASHINDWA KUVUMILIA

Soma na hizi

Tupia Comments