Habari za Mastaa

Rick Ross yuko tayari kuileta Album ya kumi “Port Of Miami 2:Born To kill”

on

Rapper Rick Ross ametangaza rasmi kuwa August 9,2019 ataachia Album yake mpya inayoitwa ‘Port Of Miami 2: Born To Kill’ na tayari ameachia trailer ya video fupi ikimuonyesha akiwa ndani ya maji mengi na kubatizwa akiwa na Padri.

Kwenye trailer hiyo Rick Ross amesikika akisema “Nilipogundua kuwa niko hai nilikaa kwenye chumba peke yangu bila Televisheni wala muziki nilisikiliza mapigo yangu ya moyo ,unasikia mapigo yangu? unaelewa sasa, ulitaka kuishi au ulizaliwa ili uwawe”

Album hiyo ‘Port Of Miami 2; Born To Kill’ imepita mikononi mwa Swizz Beatz kwenye kuitayarisha ngoma ya ‘Big Time’ inayopatikana ndani ya Album hiyo pamoja na ngoma ya ‘Act a Fool’ akiwa amemshirikisha Wale.

Rick Ross ambaye jina lake halisi ni William Leonard Roberts II ana jumla ya album tisa ambapo Album yake ya kwanza aliiachia rasmi 2006 ‘Port of Miami’ ikiwa album hii ya ‘Port of Miami 2: Born to kill” itakamilisha jumla ya Album kumi.

VIDEO: “UWOYA KAFUNGUKA “NIKO NA MPENZI, NAKULA BATA, NINA NYUMBA MBEZI BEACH”

Soma na hizi

Tupia Comments