Habari za Mastaa

Baada ya Bodyguard wa Future kupigwa hakuna shtaka lolote lililofunguliwa

on

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mpaka sasa hakuna shtaka lolote lililoripotiwa dhidi ya tukio lilomtokea bodyguard wa rapper Future ambaye alipigwa ngumi ya shingo na kuanguka siku kadhaa zilizopita nchini Hispania.

Imeelezwa kuwa Maafisa wa usalama wa raia nchini humo wameweka wazi na kusema hakuna mtu yeyote aliyekuja kufungua mashtaka dhidi ya tukio hilo na wanaamini kuwa endapo mtu angekuwa kaumizwa na kitu chochote kama silaha basi angevifata vyombo husika na kufungua mashtaka ili uchunguzi uanze kufanyike.

Hata hivyo imeripotiwa kuwa watu wa karibu na bodyguard wamedai kuwa hakutokuwa na tishio lolote kwa vijana hao waliosabisha maafa kwa sababu bodyguard huyo hana mpango wa kufungua mashtaka yoyote mahakamani na pia Rapper Future alitoa kauli ya kusema kuwa asihusishwe na kesi yoyote inayoumuhusu bodyguard wake.

VIDEO: ‘WATARAJIE NDOA, NISHAMTAMBULISHA TUNDA KWA WAZAZI ” WHOZU

Soma na hizi

Tupia Comments