Top Stories

Ujumbe wa RC Paul Makonda kwa kina mama wanaoitwa ‘Tasa’

on

Ikiwa leo ni July 12,2019 mtoto wa kwanza wa kiume wa RC Paul Makonda pamoja na mke wake anafikisha mwaka mmoja tokea azaliwe, miaka kadhaa iliyopita Paul Makonda alionyesha safari yake ya kuhangaika katika kutafuta mtoto pamoja na mke wake bila mafanikio.

Lakini leo kupitia ukurasa wa instagram wa Paul Makonda ameandika ujumbe kwa kina mama wanaohangaika kupata mtoto, walioteseka na kudharaulika na hadi wengine kufikia hatua ya kuita mpaka tasa kupitia ujumbe huo amewaomba wanawake hao wasikate tamaa.

“HAPPY BIRTHDAY MY LOVELY FRIEND OF MINE, Ninapokumbuka siku kama ya leo Kwa mwaka uliopita nayaona machozi Mengi ya furaha kwangu kwa mke wangu na ndg zangu juu ya Muujiza huu Mkubwa ktk maisha yetu”

“Kwa sababu hii naomba niseme jambo moja kwa Wakina mama wengi sana ambao wamebakia na vidonda vya kudumu moyoni baada ya morning kuchukiwa,kusingiziwa vya uongo na kutuhumiwa na ndugu au waume zao kwa kukosa watoto”

“Wengi tunasahau kuwa mtoto ni zawadi anayotupa Mungu.Wapo ambao hadi wameachwa huku wakinenewa maneno magumu ya kuvunja moyo.Leo ningependa niwape pole wote mliopitia nyakati hizi katika maisha yenu”

“Jambo kubwa ambalo ningependa kukumbusha ni kuwa pamoja na juhudi za kibinadamu za kidaktari,pamoja na maombi ya kila aina tunayoweza kufanya mbele za Mungu,pamoja na mipango mingi kuhusu kupata mtoto:JIBU LA MWISHO HUTOKA KWA MUNGU”

“Mama yangu unayepitia changamoto hii endelea kumtumaini Mungu ATAFANYA KWA WAKATI WAKE kwani yeye hawahi wala hachalewi Nakuombea kwa Mungu,Usife Moyo.Ipo siku utaitwa mama ewe ulieitwa Tasa Kwa jina la Yesu mwana wa Mungu aliye hai. Amen Ni Mimi Paul Makonda ndg yako katika Kristo”

VIDEO: VITUKO VYA SHILOLE MBELE YA SHAMSA “MWENZANGU YAMEMSHINDA SIWEZI KUMWAMBIA NG’ANG’ANA”

Soma na hizi

Tupia Comments