Habari za Mastaa

Cassper Nyovest aingiwa na wivu wa Wasanii wa Nigeria

on

Stori kubwa ambayo imeuteka mtandao wa Twitter ni kuhusu Rapper kutokea Afrika Kusini Cassper Nyovest ambaye ameweka wazi kuwa anatamani  angekuwa msanii kutokea Nigeria kutokana na umoja unaoonyeshwa kutoka kwa mashabiki pamoja na ushirikiano kati ya wasanii wao.

Cassper Nyovest alifunguka hayo kupitia mtandao wa Twitter alipoamua kumjibu shabiki yake ambaye anatokea Nigeria ambaye alimuandikia kuwa anatamani angekuwa anatokea Nchini kwake kutokana na, Cassper kuwa ni mtu mzuri, ana kipaji na huwa ni mtu wa kuongea ukweli.

“Kiukweli hata Mimi Natamani Kama ningekuwa natokea Nigeria, Upendo wanaouonesha kwa wasanii wao, Wanavyosherekea tamaduni zao, Asilimia 90 ya vitu wanavyovionesha na kuvipiga kwenye TV na Radio ni vya kwao, Wanasherekea muziki wao kila sehemu walipo duniani na wana umoja kwenye Muziki, Ndoto yangu” >>>aliandika Cassper

VIDEO: ‘WATARAJIE NDOA, NISHAMTAMBULISHA TUNDA KWA WAZAZI ” WHOZU

Soma na hizi

Tupia Comments