Mix

AUDIO:’Kuchezea elimu ya Tanzania ni hatari zaidi ya dawa za kulevya’ -Hussein Bashe

on

Moja ya habari kubwa hivi sasa Tanzania ni pamoja na hatua ya Serikali kupitia TCU kutoa orodha ya majina ya baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu wasio na sifa za kuwa wanafunzi wa vyuo.

Badhi ya watu na taasisi mbalimbali kikiwemo chuo kuku Dar es salaam UDSM kilichoikataa orodha hiyo. Kwenye Exclusive interview ya Ayo TV na millardayo.com tunaye Mbunge wa Nzega mjini Hussein Bashe ambaye na yeye ametoa ya moyoni baada ya kuiona taarifa hiyo huku akisisitiza kuwa Serikali imefanya makosa.

Bashe amesema…>>>’Tunatatizo kubwa la mfumo wa elimu kwenye nchi yetu, toka nimekuwa na ufahamu na kufuatilia mambo nimeona kila Waziri amekuwa akija na movie yake, ukijiuliza swali nani aliwadahili hawa wanafunzi jibu ni TCU‘ –Hussein Bashe

Leo mwanafunzi amekaa chuoni na katumia gharama nyingi achilia mbali matarajio yake aliyojiwekea na familia yake alafu unaenda kuzima mshumaa wake, tujiulize mara ya kwanza wakati wanadahiliwa walikuwa na sifa alafu sasa hawana sifa?‘ –Hussein Bashe

Hii inatafsiri kwamba mfumo wetu wa elimu unatatizo kubwa lakini la pili wakati unawaadhibu wanafunzi hao kwa kuwaita hawana sifa aliyewadahili umewachukulia hatua gani? leo chuo kikuu Dar es salaam wametofautiana na TCU na umeona‘ –Hussein Bashe

Mimi nasema kama Mbunge kwamba hili jambo la kuchezea elimu ya nchi hii ni hatari mno kuliko hata dawa za kulevya, kuifanya elimu hii kama ni sehemu ya kuifanyia majaribio ni hatari‘ –Hussein Bashe

Tumekuwa ni watu wa kusukumwa na matukio, Moja kati ya mtu aliyekuwa nilikuwa na matarajio makubwa sana kwenye nchi hii ni Profesa Joyce Ndalichako lakini siku zinavyokwenda naona kama anashusha viwango vya elimu ya Tanzania huyu ni mama ninayemuheshimu lakini kwa hili hatuwezi kucheza na elimu ya nchi hii‘ –Hussein Bashe

Mimi nataka nitumie fursa hii kumweleza Rais Magufuli kwamba anakila sababu ya kuwatazama watendaji wake aliyowaamini, anaweza kuwa na nia njema pamoja lakini chakutazama ni je, amewapa watu sahihi kwenye hizo nafasi?‘ –Hussein Bashe

Vipi kuhusu TCU kudaiwa kutaja majina ya wanafunzi ambao hawapo vyuoni? Bashe amesema>>’Hii inaleta tafsiri kwamba ukurupukaji uliopo ndani ya Serikali, hakuna lugha nyingine unaweza tumia na suala la kudahili ni kazi ya vyuo na TCU wao wanafanya kazi ya udalali na ni mambo ya kukurupuka‘ –Hussein Bashe

FULL VIDEO: Wema Sepetu alivyotangaza kuhamia CHADEMA, tazama kila kitu kwenye hii video hapa chini

 

Soma na hizi

Tupia Comments