Duniani

Baada ya ushujaa wa kuokoa watu 170 kwenye Ndege iliyowaka moto, Rubani kaamua haya..

on

Stori kubwa kutoka Las Vegas Marekani September 09 2015 ilikuwa ishu ya Ndege ya British Airways kuanza kuwaka moto katika Uwanja wa Ndege wakati ikiwa na abiria 159 ndani pamoja na wahudumu 13.

Ndege ilikuwa tayari imeanza safari kwenye njia ya kurukia lakini injini ya kushoto ikawaka moto, Rubani Chris Henkey ndiye aliyetoa taarifa ya kuomba msaada wa dharura huku akiendelea na jitihada za kutafuta njia ya kusimamisha ndege ili kuokoa abiria waliomo ndani ya Ndege.

Baada ya ajali hiyo, Rubani wa ndege hiyo ametangaza kwamba kwa sasa inatosha na anaona itakuwa sawa kama akistaafu >>> ‘Najua Magazeti yataniandika kunisifu kwa ushujaa lakini kulikuwa na Marubani watatu ndani ya ile ndege ambao wana mchango wao pia’- Chris Henkey.

Rubani II

Chris Henkey, Rubani aliyekuwa akirusha ndege hiyo.

Henkey alitoa taarifa ya Ndege kuwa na dharura wakati tayari Ndege iko kwenye njia ya kurukia lakini sekunde 40 mbele akaomba msaada wa Vikosi vya Zimamoto baada ya moto huo kuanza huku Ndege ikiwa bado inatembea kwenye njia ya kurukia.

Abiria 14 walitoka na majeraha madogo madogo ambayo walipata katika harakati za kujiokoa lakini hakuna abiria hata mmoja aliyefariki au kupata tatizo kubwa.

Hiki ni kipande cha Video kilichorekodiwa na walioshuhudia ndege hiyo ikiwaka moto.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments