Top Stories

BAJETI: Madiwani walipwe kila mwezi (+video)

on

“Madiwani wenzetu wanafanya kazi nzuri sana za kusimamia shughuli za maendeleo kwenye kata zetu, hawa ni Wabunge wakazi wa kwenye kata zetu ambao kila siku wako na Wananchi wetu kwenye kusimamia shughuli za maendeleo”

“Katika baadhi ya Halmashauri Madiwani wamekuwa wakikopwa posho zao na wengine hufikia hatua ya kupiga magoti kwa Wakurugenzi Watendaji ili walipwe, hii imekuwa ikipunguza ufanisi katika Halmashauri zetu kwa Madiwani wengi kufanya maamuzi yanayopendekezwa na Wakurugenzi Watendaji hata kama hayana maslahi kwa Taifa ili waweze kulipwa posho zao”

“Jambo hili limeongelewa kwa hisia kali sana na Waheshimiwa Wabunge hapa bungeni, Wabunge na Madiwani, napenda niwaeleze kuwa Mama yetu (Rais Samia) amesikia kilio chenu na alinielekeza mimi pamoja na Waziri wa TAMISEMI kulitafutia ufumbuzi suala hili”

“Napendekeza kuanzia mwaka 2021/22, Serikali Kuu ianze kulipa posho za kila mwezi za Waheshimiwa Madiwani moja kwa moja tena kwenye akaunti zao kwa Halmashauri zote zenye uwezo mdogo kimapato, Halmashauri 16 zenye uwezo mkubwa wa kimapato (Daraja A) zitaendelea kutumia mapato yake ya ndani kulipa posho za Madiwani kupitia kwenye akaunti zao”———Mwigulu

 

Soma na hizi

Tupia Comments