Mix

Kama ulimis hotuba ya Bajeti kwa mwaka 2014/2015,ipo yote hapa.

on

bungeeUna haki ya kupata chochote kinachonifikia mtu wangu wa nguvu hii baada ya kuipata nimeona haitokua nzuri kama nisiposhirikiana na wewe kuisoma,kama ilikupita hii ndiyo hotuba waweza kuisoma na wewe mtu wangu imesomwa na Mheshimiwa Mbunge Saada Mkuya.

saada

HOTUBA YA WAZIRI WA FEDHA, MHESHIMIWA SAADA MKUYA SALUM (MB) AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA FEDHA KWA MWAKA 2014/15

UTANGULIZI1. Mheshimiwa Spika, kufuatiataarif ailiyowasilishwa hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamatiya Kudumu ya Bunge ya Uchumi, Viwanda naBiashara, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lakoTukufu likubali kupokea, kujadili na kupitishaMakadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedhakwa mwaka 2014/15.

 1. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwakuniwezesha kuwasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara yamwaka 2014/15. Aidha, natoa shukrani zangu za dhatikwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuniteua kuwa Waziriwa Fedha. Ninaahidi kwamba nitatekeleza jukumu hilikwa weledi na uadilifu.

Vile vile, nawapongeza Mhe.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mhe. AdamKighoma Ali Malima (Mb) kwa kuteuliwa kuwa NaibuMawaziri wa Wizara ya Fedha. Kadhalika, namshukurupia aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha Mhe. JanethZebedayo Mbene (Mb) kwa utendaji kazi wake mahiri natunamuombea Mwenyezi Mungu ampe nguvu na afyanjema katika kazi zake mpya Wizara ya Viwanda naBiashara. Nichukue pia fursa hii kumpongeza Bw.1Rished M. Bade kwa kuteuliwa kuwa Kamishna Mkuuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.

 1. Mheshimiwa Spika, napenda kukupongeza wewemwenyewe, Naibu Spika pamoja na Wenyeviti wa Bungekwa kuongoza vyema majadiliano ya Bunge la Bajeti.
 2. Mheshimiwa Spika, naomba nitumie nafasi hiikuishukuru kwa namna ya pekee Kamati ya Kudumuya Uchumi, Viwanda na Biashara chini ya Mwenyekitiwake Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mbunge wa Kisesa)na Makamu wake Mhe. Dunstan Luka Kitandula(Mbunge wa Mkinga) kwa maoni, ushauri namapendekezo waliyoyatoa kwa Wizara wakati wakuchambua mapendekezo ya Bajeti ya Wizara ya Fedha.Aidha, nachukua nafasi hii kumshukuru Mwenyekitiwa Kamati ya Kudumu ya Bajeti Mhe. Andrew JohnChenge (Mbunge wa Bariadi Magharibi) pamoja naKamati nzima kwa ushauri wao.

Katika uandaaji wahotuba hii, Wizara imezingatia ushauri na mapendekezoya Kamati hizo pamoja na ushauri na maoni ya hojambalimbali zilizotolewa wakati wa mjadala wa bajeti yaWizara kwa mwaka 2013/14.

 1. Mheshimiwa Spika, kama unavyofahamu, Wizarailipata pigo kwa kuondokewa na kiongozi wetu mkuuMarehemuDkt.WilliamAugusta oMgimwa.Tunawashukuru Viongozi wa Serikali, WaheshimiwaWabunge, Washirika wa Maendeleo, Taasisi mbalimbalipamoja na wananchi kwa ushirikiano waliotupa kipindichote cha msiba. Tumeendelea kuenzi misingi imaraaliyotujengea marehemu katika kutekeleza majukumuya Wizara. Aidha, tunapenda kutoa pole kwa ndugu na2jamaa kufuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wa ChalinzeMarehemu Saidi Ramadhani Bwanamdogo. MwenyeziMungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi.Amina.
 • Mheshimiwa Spika, napenda kuwapongeza, Mhe.Yusuf Salim Hussein Mbunge wa Chambani, Mhe.Godfrey William Mgimwa (Mbunge wa Kalenga) na Mhe.Ridhiwani Jakaya Kikwete (Mbunge wa Chalinze) kwakuchaguliwa kwao.

 • Mheshimiwa Spika, kwa namna ya kipekeenapenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa Mhe.Mizengo Peter Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania na Mbunge wa MpandaMashariki kwa hotuba yake nzuri ambayo imetoamwelekeo wa shughuli za Serikali kwa mwaka 2014/15.

 • Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu nitaanzakuelezea mapitio ya utekelezaji wa mipango ya Wizarakatika mwaka 2013/14. Nitaelezea pia mikakatimbalimbali ambayo Wizara imeweka kwa mwaka2014/15 ili kuendelea kuboresha utekelezaji wamajukumu yake ya msingi yakiwemo: usimamizi waBajeti ya Serikali; ukusanyaji mapato ya Serikali;usimamizi wa misaada na mikopo; ulipaji wa Deni laTaifa; usimamizi wa matumizi ya fedha za umma;usimamizi na udhibiti wa ununuzi wa umma;usimamizi wa utekelezaji wa MKUKUTA; na usimamiziwa mashirika na taasisi za umma.

 • Mheshimiwa Spika, mwisho nitawasilisha bajetiya mwaka 2014/15 kwa mafungu saba ya wizara yafedha ambayo ni fungu 7, 10, 13, 21, 22, 23 na fungu50 pamoja na fungu 45 la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali.

 • MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETIYA WIZARA KWA MWAKA 2013/14 NA MALENGO YAMWAKA 2014/15

  1. Mheshimiwa Spika, uandaaji, utekelezaji nausimamizi wa Mpango na Bajeti ya Wizara umezingatiamalengo ya Mpango Mkakati wa Wizara wa mwaka2012/13 – 2016/17 ambao utaiwezesha Wizara kufikiamalengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2025;Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2011/12 -2015/16; Mkakati wa Kukuza Uchumi na KupunguzaUmaskini Tanzania (MKUKUTA II); Malengo yaMaendeleo ya Milenia 2015; Mkakati wa Pamoja waMisaada Tanzania (MPAMITA) pamoja na Programu yaMaboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma – PFMRP.Aidha, Mpango na Bajeti ulizingatia Ilani ya Uchaguziya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 pamoja naMfumo wa Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa (BigResults Now – BRN).
 • Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2013/14,Wizara ilipanga kutekeleza yafuatayo: kuongeza mapatoya ndani kufikia uwiano wa Pato la Taifa wa asilimia20.9 kwa mwaka 2013/14 ikilinganishwa na asilimia17.7 kwa mwaka 2012/13; kukamilisha Ripoti za Utafitiwa Mfumo Bora wa Kodi wa Serikali ya Jamhuri ya4Muungano wa Tanzania; kuandaa na kusimamiautekelezaji wa bajeti ya Serikali; kusimamia utekelezajiwa MKUKUTA-II; kufanya ukaguzi wa miradi yamaendeleo na kutoa ushauri wa kitaalamu kwawatekelezaji wa miradi hiyo; kukamilisha Sera ya Maliya Umma; kufanya tathmini yausimamizi nautekelezaji wa malipo ya mishahara ya watumishi waumma; kusimamia utekelezaji wa mipango kazi yaukaguzi na uzingatiwaji wa miongozo ya ukaguzi katikaWizara, Idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali, naMamlaka ya Serikali za Mitaa; kuratibu na kusimamiaupatikanaji wa misaada na mikopo nafuu kutoka NchiWahisani, Mashirika na Asasi za Fedha za Kimataifa;kuidhinisha miradi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma naBinafsi (PPP); na kukamilisha Sera ya Taifa ya Ununuziwa Umma.

 • Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Wizarapia ilipanga kukamilisha miradi ya MCA-T na kukabidhimiradi iliyokamilika kwa taasisi husika; kusimamiautekelezaji wa Mpango Mkakati wa Programu yaMaboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu yanne (PFMRP IV); kufanya uhakiki wa Wastaafu waliopokatika Daftari la Pensheni la Hazina; kuunganishaHazina Ndogo na Sekretarieti za Mikoa 24 katika mfumowa malipo kwa njia ya elektroniki kupitia Benki Kuu yaTanzania (Tanzania Inter- Bank Settlement System -TISS); kuimarisha utendaji kazi wa Ofisi ya Msajili waHazina; na kuandaa na kuhuisha kanuni na miongozoya utekelezaji wa Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramuna Ufadhili wa Ugaidi.5Mfumo wa Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,kupitia Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa, Wizaraya Fedha katika maabara ya utafutaji wa rasilimalifedha iliwekewa malengo yafuatayo: kuongeza mapatomapya ya kodi ya shilingi trilioni 1.16; kuongezamapato mapya yasiyo ya kodi ya shilingi bilioni 96.7;kudhibiti matumizi; na kutafuta fedha za utekelezaji wamiradi ya Tekeleza Sasa kwa Matokeo Makubwa katikasekta zinazotekeleza miradi hiyo.

 • Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili 2014,ukusanyaji wa mapato kutoka vyanzo vilivyoibuliwachini ya BRN umefikia shilingi bilioni 338 sawa naasilimia 29.14 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni1.16. Matokeo yasiyoridhisha yalisababishwa na baadhiya mapendekezo ya BRN kutokutekelezwa katikamwaka 2013/14. Mapendekezo hayo ni kubadilishamfumo wa ushuru wa bidhaa zisizo za petroli kutokaspecific kwenda advalorem (makisio shilingi bilioni 386)na kuanzisha kodi ya zuio ya asilimia tano kwenyebidhaa zinazotoka nje ya nchi (makisio shilingi bilioni225.6). Kwa vile ukusanyaji wa mapato ndio msingi wakufanikiwa kwa BRN, Serikali inachambua vyanzombadala vya kufidia mapato haya ili kuhakikisha lengokuu la kuongeza mapato kwa shilingi trilioni 3.48linafikiwa ifikapo mwaka 2015/16.6Mwenendo wa Uchumi.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Benki Kuu iliendelea na jukumu lakuandaa, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa seraya fedha inayolenga kuwa na kiwango kidogo chamfumuko wa bei kwa ajili ya kuhakikisha gharama zamaisha haziongezeki. Kutokana na juhudi hizi,mfumuko wa bei umeshuka kutoka wastani wa asilimia16 mwaka 2012 hadi kufikia wastani wa asilimia 7.9mwaka 2013. Katika kipindi hiki uchumi umeendeleakuimarika huku ukuaji halisi wa Pato la Taifaukiongezeka kwa asilimia 7.0 katika kipindi cha mwaka2013 ikilinganishwa na asilimia 6.9 katika mwaka2012. Shughuli za kiuchumi zilizokua kwa kiasikikubwa ni pamoja na mawasiliano asilimia 22.8,huduma za kifedha asilimia 12.2, ujenzi asilimia 8.6, nauuzaji bidhaa wa jumla na rejareja asilimia 8.3. Katikamwaka 2014/15, Wizara kupitia Benki Kuu itaendeleakushirikiana na wadau wote katika kuhakikishakwamba lengo la msingi la utulivu wa bei na ukuaji wauchumi linadumishwa.Uandaaji na Usimamizi wa Utekelezaji wa Bajeti yaSerikali

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara imeratibu uandaaji wa Mwongozo wa Mpango naBajeti kwa kipindi cha 2014/15 – 2016/17 kwa Wizara,Idara zinazojitegemea, Mikoa na Mamlaka za Serikali zaMitaa na kusambaza kwa wadau mwezi Desemba kama7ilivyopangwa. Aidha, Wizara imeandaa na kuchapishavitabu vya bajeti ya Serikali vya mwaka 2014/15(Volume I, II, III na IV) kama vilivyowasilishwa Bungenikwa ajili ya mjadala wa Bunge la Bajeti la mwaka2014/15 unaoendelea; kitabu cha tafsiri rahisi ya bajetiya Serikali (Citizen’s Budget) kwa mwaka 2013/14; naKitabu cha Budget Background and Medium TermFramework – 2013/14 – 2015/16.

 • Mheshimiwa Spika, Serikali inakusudia kuanzakutumia mfumo wa Programu katika uandaaji,uidhinishaji na utekelezaji wa Bajeti. Mfumo huuutasaidia Serikali kugawa rasilimali kwa kuzingatiamatokeo na kuweka viashiria vya kufikia malengo.Katika hatua za awali za maandalizi ya utekelezaji wamfumo huu katika mwaka 2013/14, Wizara ilitengafedha kwa ajili ya mafunzo kwa wataalam wa Wizaranane za mfano. Maandalizi haya ya kimkakati nakimfumo yataendelea katika mwaka 2014/15. Wizarazilizotengwa kwa majaribio na ambazo tayarizimefanyiwa mafunzo ni Wizara ya Maji, Wizara yaUjenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Elimu naMafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,Wizara ya Kilimo, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsiana Watoto na Wizara ya Fedha. Wizara hizi kwa sasazinaendelea na zoezi la kuandaa programu na viashiriavya kupima utekelezaji kabla ya mfumo kuanzakutumika.

 • Mheshimiwa Spika, Wizara iliratibu kikao kazicha wataalamu wa wizara, mikoa na halmashaurikuhusu mfumo wa ufuatiliaji, tathmini na utoaji wataarifa za utekelezaji wa Bajeti. Katika kipindi hicho,8Wizara pia ilifanya kikao kazi kilichohusisha washirikikutoka wizara, idara za Serikali zinazojitegemea, mikoana Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa lengo lakutathmini uandaaji na uwasilishwaji wa Bajeti yaSerikali kwa mwaka 2012/13 na kufanya mkutano wamwaka wa wadau ambao ulijumuisha Washirika waMaendeleo kwa lengo la kutathmini utekelezaji waBajeti ya Serikali.

 • Mheshimiwa Spika, katika kusimamia nakudhibiti utekelezaji wa bajeti ya Serikali ikiwemokufuatilia matumizi ya fedha za umma, Wizara ilifanyaufuatiliaji na ukaguzi wa matumizi ya fedha zilizotolewakwa ajili ya maendeleo kwa miradi ya ASDP na DASIPikihusisha wizara nne, mikoa sita na halmashauri 33.Aidha, ufuatiliaji na ukaguzi ulifanyika kwa mapato namatumizi ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Taifa yaChakula (NFRA) na kwa fedha zilizotolewa kuhudumiavituo 16 vya Makazi ya Wazee katika mikoa 14 nchini.

 • Mheshimiwa Spika, katika ukaguzi huo, Wizarailibaini kuwapo kwa upungufu na changamoto katikamaeneo haya ikiwa ni pamoja na: fedha kutowafikiawalengwa kwa wakati kama ilivyopangwa; udhaifukwenye udhibiti wa ndani wa matumizi na hivyokusababisha kuwapo kwa huduma duni; na miradikutokamilika kwa wakati na kuwepo kwa bakaa yafedha za maendeleo. Aidha, zimekuwepo changamoto zakubadilika mara kwa mara bei ya kununulia nafaka nagharama za usafirishaji, hivyo kuathiri malengoyaliyopangwa ikiwemo kusababisha madeni. Wizaraimewasiliana na wahusika na kutoa nyaraka zamaelekezo ya kuhakikisha kwamba udhibiti wa ndani9wa matumizi unaimarishwa katika ngazi zote zausimamizi na inapobidi hatua za kisheria zichukuliwekwa wahusika.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara inatarajia kutekeleza yafuatayo: kupitia mfumowa uwasilishaji wa bajeti za wizara, idara za Serikali,mikoa na halmashauri na kuhakikisha kuwa sera namipango ya kitaifa na ile ya kisekta vyote vimezingatiwaipasavyo katika Bajeti ya Serikali na kutengewa fedha;kufanya tathmini ya utekelezaji wa Bajeti ya Serikali,kuendelea kuboresha mfumo wa mpangilio wa Bajeti yaSerikalikwakuzingatiaprogram umbalimbali;kuimarisha mifumo ya kompyuta ya uandaaji bajeti ilikukidhi mahitaji ya taarifa mbalimbali zinazohitajika;kuendelea kujenga uwezo wa wizara, idara za Serikali,mikoa na halmashauri katika uandaaji wa Bajeti yaMuda wa Kati, usimamiaji wake na utoaji taarifa zautekelezaji ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji na tathminikwa wakati; kutayarisha taarifa mbalimbali zautekelezaji wa Bajeti ya Serikali ili kuhakikisha uwazina uwajibikaji unazingatiwa; na kufuatilia matumizi yafedha za umma zikiwemo fedha za mishahara, matumizimengineyo na fedha za miradi.Usimamizi wa Misaada na Mikopo

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara ilifanikisha kusainiwa kwa mikataba 18 kwa ajiliya misaada na mikopo nafuu yenye thamani ya jumlaya shilingi bilioni 958.027 kutoka kwa Washirika waMaendeleo. Aidha, Wizara imeendelea kuratibuukamilishaji wa Mwongozo mpya wa Ushirikiano wa10Maendeleo – Development Cooperation Frameworkambao utachukua nafasi ya Mkakati wa Pamoja waMisaada Tanzania (MPAMITA). Mwongozo huu unalengo la kusimamia ushirikiano wa maendeleobaina ya Serikali na Wadau wa Maendeleo nakuendeleza mafanikio yaliyopatikana wakati wautekelezaji wa MPAMITA. Lengo la ujumla nikupatikana ufanisi katika misaada kutoka kwaWashirika wa maendeleo na kubainisha wajibu wakila mdau wa maendeleo wakiwemo raia, wabunge,asasi zisizo za kiserikali na sekta ya habari.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kufanya yafuatayo: kuzinduaMwongozo wa Ushirikiano wa Maendeleo na kuandaampango kazi wake pamoja na kuhamasisha matumiziyakekwa Washirika wa Maendeleo, Wizara, IdaraZinazojitegemea, Serikali za Mitaa, Taasisi Binafsi naWaheshimiwaWabunge; kutathmini utekelezaji wamiradi na programu mbalimbali inayotekelezwa kwafedha toka Washirika wa Maendeleo kwa nia yakuhakikisha kwamba thamani ya fedha inapatikanakatika miradi hiyo; kushiriki kwenye majadiliano naJumuiya za kikanda na kimataifa; na kuendeleakutafuta fedha za misaada na mikopo nafuu kwa ajili yautekelezaji wa miradi ya maendeleo, na Misaada yaKiufundi kutoka kwa Mashirika ya Kimataifa na nchiwahisani.11Ulipaji wa Deni la Taifa

 • Mheshimiwa Spika, Deni la Taifa limeendeleakusimamiwa na Sheria ya Madeni ya mwaka 1974 namarekebisho yake ya mwaka 2004. Wizara imeendeleakutoa kipaumbele katika ulipaji wa madeni kwa wakatiili kuepuka malimbikizo ya riba. Katika kipindi chaJulai, 2013 hadi Aprili, 2014 malipo ya deni la ndaniyalifikia shilingi bilioni 1,694.53 ambapo kati ya malipohayo riba ni shilingi bilioni 581.20 na Mtaji (principalrollover) ni shilingi bilioni 1,113.33. Aidha, deni la njelimelipwa kwa kiasi cha shilingi bilioni 340.22, kati yakiasi hicho malipo ya riba ni shilingi bilioni 201.52 nadeni halisi – principal ni shilingi bilioni 138.70.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kulipa madeni ya ndani na nje kwawakati ikiwa ni pamoja na kulipa kwa wakati madenimbalimbaliambayoserikali imeingiamikataba(Contractual Liabilities) na madai ya dharura(Contingent Liabilities) pindi yanapotokea.Usimamizi wa Matumizi ya Fedha za Umma

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kujengauwezo wa usimamizi wa matumizi ya fedha za ummakwa kudhamini mafunzo ya muda mrefu kwawatumishi 313 wa kada ya uhasibu, ugavi na kompyutakutoka kwenye wizara, idara za serikali, sekretariati zamikoa,manispaa, halmashauri za miji na wilayawaliopo vyuoni na watumishi 218 walipewa mafunzo yamuda mfupi kwa lengo la kuongeza ufanisi katikausimamizi wa matumizi ya fedha za umma. Aidha,12Wizara imeendelea kusambaza Mfumo wa Malipo waKielektroniki -TISS mikoani ambapo hadi sasa jumla yamikoa 20 imeunganishwa katika mtandao huo. Mikoailiyounganishwa kwenye mtandao huo ni Iringa,Morogoro, Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Mbeya, Rukwa,Ruvuma, Lindi, Simiyu, Mwanza, Kagera, Geita, Mara,Mtwara, Kigoma, Shinyanga, Njombe, Dar es Salaam naKatavi. Vile vile, mikoa mipya ya Geita, Simiyu, Katavina Njombe imeunganishwa kwenye mtandao wa malipowa Serikali (Intergrated Financial Management System).

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea nampango wa kutekeleza mfumo wa uandaaji wa taarifaza hesabu kwa kuzingatia Viwango vya Kimataifa vyaUandaaji wa Taarifa za Hesabu katika Sekta ya Umma -IPSAS Accrual Basis ambapo hesabu za majumuisho zamwaka 2012/13 zimeandaliwa kwa kutumia mfumohuo kwa mara ya kwanza na kuwasilishwa kwaMdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwawakati.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,pamoja na mambo mengine, Wizara itaendeleakuboresha usimamizi wa fedha za umma kwa kufanyayafuatayo: kuendelea kutoa udhamini wa masomo yamuda mrefu na mfupi kwa wahasibu, wakaguzi,maafisa ugavi na wataalamu wa kompyuta kutokaSerikali Kuu na serikali za mitaa; kuweka mitambokatika hazina ndogo zote ili kuwezesha sekretariati zamikoa na hazina ndogo kufanya malipo kwa kutumiamifumo ya malipo ya kielektroniki -TISS/EFT;13kuendelea kutoa mafunzo ya TISS/EFT kwa wahasibuna watumishi wa kada zingine ili kuimarisha mfumo wamalipo; na kuanza ujenzi wa jengo la ofisi ya HazinaNdogo Arusha.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15 ilikuinua kiwango cha fani ya uhasibu sambamba nakuimarisha usimamizi wa fedha za umma Tanzaniaitakuwa mwenyeji wa mkutano wa Wahasibu Wakuu waSerikali wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika –ESAAG.Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha zaUmma – Public Finance Management ReformProgramme (PFMRP)

 • Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Programu yaMaboresho ya Usimamizi wa Fedha za Ummaimekamilisha utafiti wa mfumo wa kupeleka fedhakwenye Serikali za Mitaa, mpango wa utekelezaji wautafiti huo umeandaliwa na utekelezaji wake utaanzamwaka wa fedha 2014/15. Aidha, utafiti juu ya mifumoya fedha inayotumiwa na Serikali kwa lengo lakuiunganisha mifumo hiyo ili kuboresha usimamiziwake umekamilika. Vile vile, Wahasibu 522 kutokaWizara mbalimbali, hazina ndogo na sekretarieti zamikoa walipata mafunzo juu ya Viwango vya Kimataifavya Uandaaji wa Taarifa za Hesabu katika Sekta yaUmma na watumishi wengine 34 ambao wanasimamiaprogramu hii kutoka katika wizara na taasisi walipatamafunzo ya kusimamia Mabadiliko na Kuandaa14Mipango Mkakati -Change Management and StrategicPlanning. Mafunzo haya yalilenga kuwajengea uwezo wakuandaa mipango na bajeti inayolenga katikakutekeleza maboresho ya usimamizi wa fedha za umma.

 • Mheshimiwa Spika,katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kuboresha usimamizi wa fedha zaumma kwa kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Nneya Programu ya PFMRP kwa kufanya yafuatayo: kupitiana kuboresha mifumo ya kifedha na kuangalia njia boraya kuiunganisha baada ya utafiti kukamilika;nakuwajengea uwezo wakaguzi wa ndani katika wizara,idara, wakala za Serikali na halmashauri za Serikali zaMitaa juu ya ukaguzi wa mifumo ya fedha, usimamizina ukaguzi wa vihatarishi, ukaguzi wa bajeti namishahara, na ukaguzi wa miradi.Sera ya Ununuzi wa Umma

 • Mheshimiwa Spika, katika kusimamia Sekta yaUnunuzi wa Umma nchini, Wizara imeendeleakutekeleza yafuatayo:kuandaa Sera ya Taifa yaUnunuzi wa Umma; kuandaa mapendekezo ya muundowa Vitengo vya Usimamizi wa Ununuzi na UgaviSerikalini; na kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzokwa maafisa ununuzi na ugavi walioko katika Mamlakaza Serikali za Mitaa; na kuendelea kuhuisha taarifa zamaafisa ununuzi na ugavi Serikalini, ambapo taarifa zamaafisa 332 katika mikoa ya Shinyanga, Kagera,Mwanza na Mara zimehakikiwa na kuingizwa katikadaftari la maafisa ununuzi na ugavi.15

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kufanya yafuatayo: kuandaa Mkakatiwa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Ummana kusimamia utekelezaji wa Sera hiyo; kuhuishamuundo wa vitengo vya usimamizi wa ununuzi na ugaviserikalini; kuipitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Na.7ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013;kukamilisha tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwamaafisa ununuzi na ugavi Serikalini; na kufanyatathmini juu ya ufanisi wa ununuzi wa umma nchini.Udhibiti wa Ununuzi wa Umma

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi waUmma imetoa mafunzo kuhusu sheria, kanuni nataratibu za ununuzi kwa taasisi za umma 32 ambapowatumishi 747 walihudhuria mafunzo hayo. Aidha,Mamlaka ilitoa mafunzo kuhusu mfumo wa upokeaji nausimamizi wa taarifa za ununuzi nchini katika vituovinne vya Morogoro, Arusha, Mwanza na Mbeya ambapojumla ya washiriki 330 kutoka taasisi 191 walishiriki.Vile vile, Mamlaka imeendelea kusimamia mfumo waupokeaji na usimamizi wa taarifa za ununuzi nchiniambapokatikakipindihicho ,taasisi191ziliunganishwa na kupatiwa mafunzo ya kutumiamfumo huo na hivyo kufanya jumla ya taasisizilizounganishwa na kupatiwa mafunzo kufikia 364,sawa na asilimia 80 ya taasisi zote.16

 • Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mamlaka yaUdhibiti wa Ununuzi wa Umma imefanya ukaguzikuhusu utoaji wa zabuni na utekelezaji wa mikatabaitokanayo na ununuzi wa umma katika Taasisi 120zikiwemo wizara na idara zinazojitegemea 32, mashirikaya umma 46 na serikali za mitaa 42. Ukaguzi huuuilihusisha mikataba 5,867 yenye thamani ya shilingibilioni 1,985.427 ikiwemo miradi 207 ya ujenzi yenyethamani ya shilingi bilioni 777.2. Ripoti ya ukaguziinaonesha wastani wa uzingatiwaji wa sheria yaununuzi ulikuwa ni asilimia 64 ambayo ni chini yalengo la asilimia 80. Maeneo yaliyobainika kuwa naudhaifu mkubwa ni katika usimamizi wa mikataba nautunzaji wa nyaraka za ununuzi.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kutekeleza yafuatayo: kuandaampango kazi wa usimamizi wa utekelezaji wa Sheria yaUnunuzi wa Umma ya Mwaka 2011; kuelimisha wadaumbalimbali kuhusu Sheria mpya na kanuni zake;kuendelea na maandalizi ya kuanzisha mfumo waununuzi kwa njia ya kielektronic (e-procurementsystem); kufungua ofisi za kanda Dodoma, Mbeya naMwanza; kushirikiana na TAMISEMI ili kukabiliana nachangamoto zilizopo kwenye vitengo vya ununuzi vyahalmashauri mbalimbali; kufanya kazi na Asasi zaKiraia na Wanahabari ili kuongeza uelewa wa masualaya Ununuzi wa Umma kwa wananchi; na kuendeleakusimamia ununuzi katika sekta ya Umma.17Huduma ya Ununuzi Serikalini

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Wakala wa Huduma ya UnunuziSerikalini imetekeleza yafuatayo: kuongeza vifaa vyahuduma mtambuka kutoka 86 vilivyokuwepo hadi 181;kuendelea na ujenzi wa Ofisi na ghala katika mkoa waManyara; kuendelea na ujenzi wa kituo cha mafutamkoa wa Dodoma; na kununua magari mawilimakubwa yenye uwezo wa kubeba lita 45,000 za mafutakila moja kwa ajili ya kusafirisha mafuta toka kwawazabuni kwenda mikoani. Aidha, Wakala wa Hudumaya Ununuzi Serikalini, imeanza kufunga Mfumo waUdhibiti na Usimamizi wa Mafuta ya Magari ambaoutaanza kwa majaribio Agosti, 2014 katika mkoa waDar es Salaam ili kudhibiti matumizi ya mafuta katikamagari ya Serikali.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Wakala wa Huduma ya UnunuziSerikalini imepanga kutekeleza yafuatayo: kukamilishakazi ya kufunga Mfumo wa Udhibiti na Usimamizi waMafuta ya Magari katika mikoa ya Arusha, Mwanza,Dodoma, Iringa na Mbeya; kuanza kazi za Ujenzi waOfisi katika mikoa ya Njombe na Mara; kukamilishaujenzi wa visima vya mafuta katika mikoa ya Geita,Katavi na Wilaya ya Ileje; na kuongeza uwezo wakuhifadhi mafuta kufikia wastani wa lita 50,000 katikavituo vya mikoa ya Arusha, Mwanza, Kigoma, Mtwara,Lindi, Tabora, Pwani, Tanga na Ruvuma. Aidha, Wakalawa Huduma ya Ununuzi Serikalini itahuisha muundowake ili kuweza kutoa huduma ngazi ya wilaya na18kuanza kutekeleza utaratibu wa ununuzi wa magarikwa pamoja.Rufaa za Zabuni za Umma

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma imepokea jumlaya mashauri35, kati ya hayo mashauri matatuyaliondolewa na walalamikaji kabla ya kusikilizwa;mashauri 17 walalamikaji walishinda; mashauri 11walalamikaji walishindwa; mashauri mawili yalifutwakufuatana na sheria; shauri moja halikutolewa uamuzikutokana na ukomo wa muda wa kulisikiliza; na shaurimoja lipo kwenye hatua ya kusikilizwa. Aidha, katikamwaka 2014/15, Mamlaka itaendelea kusikiliza nakutolea maamuzi malalamiko na rufaa katika Ununuziwa Umma na kuelimisha umma na wadau juu yakuwasilisha pingamizi za zabuni kwa mujibu wa Sheriaya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011.Usimamizi wa Mali ya Serikali

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara iliendelea kuandaa Sera ya Mali ya Umma.Lengo la sera hii ni kusimamia na kutoa miongozo yaudhibiti wa mali ya umma. Aidha, Wizara ilifanyauthamini wa mali ya Serikali katika mikoa mitano nawizarambili,hivyokufanyawiza ra,idarazinazojitegemea na wakala wa Serikali zilizofanyiwauthamini kufikia 42. Katika kipindi hicho, usimikaji wamfumo wa uhakiki wa mali ya umma ulikamilika. Vilevile, Wizara iliendelea na zoezi la kuondosha mali19chakavu katika wizara na idara za Serikali ambapojumla ya shilingi bilioni 1.58 zilikusanywa kutokana namauzo ya vifaa hivyo na shilingi milioni 12.83 kutokanana utoaji wa leseni za udalali.

 • Mheshimiwa Spika, Wizara ilifanya uhakiki wamali ya Serikali katika wizara, idara zinazojitegemea nawakala za Serikali kwa lengo la kudhibiti matumizi yamali katika taasisi hizo. Aidha, Wizara imefanya uhakikimaalum katika Bohari Kuu ya Madawa ambapo ushauriulitolewa wa namna ya kupunguza hasara inayotokanana madawa, vifaa tiba na vitendanishi kuisha mudawake wa matumizi kabla ya kutumika.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka, 2014/15,Wizara imepanga kukamilisha Sera ya Mali ya Ummana kuisambaza kwa wadau kwa ajili ya kupata maonikabla ya kuanza utekelezaji wake. Aidha, Wizaraimepanga kufanya uthamini wa mali katika mikoa sabana taarifa zake kuingizwa kwenye Daftari la Mali yaSerikali. Vile vile, Wizara itaendelea kuondosha malichakavu, mali zilizokwisha muda wake na vifaa sinziakwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Fedha za Umma;kushughulikia taarifa za ajali na potevu za mali yaSerikali;nakuendeleakuchambu a,kufanyamajadiliano na wadai na kulipa madai ya fidia na kifutamachozi yanayotokana na amri ya Mahakama.Kadhalika, Wizara itaendelea na uhakiki wa mali katikawizara, idara zinazojitegememea na wakala za Serikali.Mpango wa MilleniumTanzania (MCA-T)20ChallengeAccount–

 • Mheshimiwa Spika, Programu ya MilleniumChallenge Account Tanzania iliendelea na ukamilishajiwa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji,nishati ya umeme na maji. Miradi yote ya barabaraimekamilika isipokuwa sehemu ya Laela- Sumbawangakatika barabara ya Tunduma- Sumbwanga ambayoinatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka2014. Miradi ya umeme na maji imekamilika na ipokatika kipindi cha uangalizi. Aidha, kutokana nautekelezaji wa kuridhisha, Tanzania imekidhi vigezo nahivyo itanufaika na awamu ya pili ya msaada waSerikali ya Marekani kupitia Shirika lake laChangamoto za Milenia (MCC). Katika awamu ya pili,miradi itakayofadhiliwa ni ya umeme na barabara zavijijini Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.Ukaguzi wa Ndani

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara imetekeleza yafuatayo: kutoa Mwongozo waKamati za Ukaguzi katika Sekta ya Umma kwa lengo lakuhakikisha utendaji wenye tija kwa Kamati zote zaUkaguzi; kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezowakaguzi wa ndani 458, wajumbe wa Kamati zaUkaguzi na wadau wa ukaguzi wa ndani wapatao 567;kufanya ukaguzi wa miradi ya maendeleo 11; ukaguziwa orodha ya malipo ya mishahara; na kuhakiki madaimbalimbali yaliyowasilishwa wizarani kabla ya kulipwa.21

 • Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi zaSerikali za kudhibiti ubora wa utekelezaji wa miradimbalimbali ya maendeleo, Wizara imenunua vifaa vyakuhakiki ubora wa miundombinu. Vifaa hivyovitatumika katika ukaguzi wa miradi inayotekelezwa naWizara, Idara, Wakala za Serikali na Halmashauri zaSerikali za Mitaa katika kuhakikisha kuwa miradi namiundombinu inayotekelezwa inakuwa na uboraunaokidhi viwango na hatimaye kupata thamani yafedha. Hatua hii itaenda sambamba na kuwajengeauwezo wakaguzi wa ndani Serikalini katika kufanyaukaguzi wa kiufundi kwa miradi inayotekelezwa katikataasisi zao.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kusimamia kada ya ukaguzi wa ndanina kamati za ukaguzi; kufanya ukaguzi wa Mfumo waulipajiMishaharaSerikalini;k uhakikimadaimbalimbali ya Serikali kabla ya kuyalipa; na kufuatiliautekelezaji wa miongozo mbalimbali iliyotolewa. Aidha,Wizara inatarajia kutoa miongozo ifuatayo: Mwongozowa Usimamizi wa Viashiria Vya Udanganyifu; Mwongozowa Udhibiti wa Ndani; Mwongozo wa Ufuatiliaji naTathmini ya Usimamizi wa Vihatarishi; Mwongozo waUkaguzi wa Ununuzi; na Mwongozo wa Ukaguzi waMikataba. Vile vile, wizara kwa kushirikiana na Taasisiza Serikali itaendelea kuimarisha ofisi za MkaguziMkuu wa ndani kwa lengo la kusimamia matumizi yafedha.Ukaguzi wa Hesabu za Serikali22

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Ofisiya Taifa ya Ukaguzi imetekeleza kazi zake kwa mujibuwa sheria. Ofisi imeendelea kuwa mshirika katika Bodiya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa katika kukagua taasisiza Umoja wa Mataifa. Aidha, Ofisi imeendesha mafunzokwa Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu za Serikalina Kamati ya Bajeti kwa lengo la kuzijengea uwezo wakuimarisha uwajibikaji na utawala bora. Vile vile,ukaguzi wa mapato na matumizi ya vyama vya siasavyenye usajili wa kudumu unaendelea.

 • Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuondoawakaguzi katika majengo ya wakaguliwa, Ofisi ya Taifaya Ukaguzi imekodi majengo ya ofisi katika mikoa yaMwanza, Tabora, Tanga, Iringa, Kagera na Geita. Aidha,ujenzi wa ofisi katika mkoa wa Dodoma unaendeleaukiwa katika hatua za mwisho. Vile vile, Ofisiimeendelea na uunganishaji wa ofisi zake zilizokomikoani na makao makuu kwa njiaya mtandaompana. Kwa mwaka huu ofisi 4 zimeunganishwa nahivyo kufanya ofisi zilizounganishwa kufikia 14.

 • Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15, Ofisiinatarajia kufanya yafuatayo: kukagua mafungu yote 49ya Wizara na Idara za serikali, hesabu za Mikoa yote 25ya Tanzania Bara, Hesabu za Halmashauri zote 161 zaWilaya, Miji, Manispaa na Majiji, Mashirika ya Umma177, Balozi zote 32 zilizoko nje ya nchi na Wakala 33 zaSerikali pamoja na kufanya ukaguzi wa thamani yafedha katika maeneo sita; kuendelea na ukaguzi wamapato na matumizi ya vyama vyote vya siasa; kuanzaukaguzi katika sekta ya gesi na mafuta pamoja na23ukaguzi wa miradi mikubwa inayoendeshwa kwa ubiawa sekta ya Umma na Sekta binafsi; kuendeleakushiriki kikamilifu katika jukumu la kukagua taasisiza Umoja wa Mataifa sanjari na wanachama wenginewanaounda Bodi ya Ukaguzi ya Umoja wa Mataifa.

 • Mheshimiwa Spika,mambomengineyatakayoteke lezwa katika mwaka 2014/15, ni pamojana: kuendelea na zoezi la kuwaondoa wakaguzi katikamaeneo ya wakaguliwa katika wizara zote na katikamikoa 6 iliyobaki; kuendelea kuzijengea uwezo kwa njiaya mafunzo Kamati za Kudumu za Bunge za Hesabu zaSerikali na Kamati ya Bajeti katika maeneo ya kuelewakwaundanitaarifazaukagu ziwahesabuzinazoandaliwa na wakaguliwa; kukamilisha ujenzi waofisi katika mkoa wa Rukwa pamoja na kuanza ujenziwa ofisi katika mikoa ya Mara na Iringa; na kutoamafunzo kwa watumishi ili kuimarisha uwezo waokatika kutumia mfumo wa TeamMate ili kuendana namabadiliko ya teknolojia katika ukaguzi wa kisasa.Uratibu wa Utekelezaji wa MKUKUTA

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuratibuutekelezaji wa MKUKUTA II kwa kufanya ufuatiliaji,tafiti, na tathmini na kuandaa taarifa ya utekelezaji nahali ya Umaskini nchini ili kuwezesha maamuzi yakisera, kibajeti na kiutekelezaji. Kazi ya uandaaji waTaarifa ya Mwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA IIimekamilika na kuwekwa katika tovuti ya Wizara.Aidha, Wizara inaendelea kukamilisha Taarifa ya24Maendeleo ya Malengo ya Milenia. Taarifa ya awaliinaonesha kuwa umaskini wa mahitaji ya msingi kwaTanzania Bara ni asilimia 28.2 ambapo kwa Dar esSalaam ni asilimia 4.2, maeneo mengine ya mjini niasilimia 21.7 na maeneo ya vijijini ni asilimia 33.3.Umaskini wa chakula ni asilimia 9.7 ambapo kwa Dares Salaam ni asilimia 1.0, maeneo mengine ya mjini niasilimia 8.7 na maeneo ya vijijini ni asilimia 11.3.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara imepanga kutekeleza yafuatayo: kukusanya nakuchambua taarifa mbalimbali kutoka katika Wizara,Idara na Wakala za Serikali ili kuandaa Taarifa yamwaka ya Utekelezaji wa MKUKUTA II; kuandaa taarifaya mwisho ya kutathimini utekelezaji wa Malengo yaMaendeleo ya Milenia; kufanya mapitio ya MKUKUTA II;kukamilisha Mpango wa Utekelezaji wa Kinga ya Jamiipamoja na kuainisha viashiria vya upimaji juhudi zakinga ya jamii; na kuratibu mkutano wa kitaifa wakujadili sera za kupambana na Umaskini nchini. PiaWizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbaliinaandaa mapendekezo ya hatua zitakazofuata baadaMKUKUTA II kufikia kikomo mwezi Juni, 2015.

 • Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Mradi waSELF II imeendelea kutoa mikopo kwa wajasiriamaliambapo hadi kufikia Aprili 2014, mikopo yenye thamaniya shilingi bilioni 8.6 ilikopeshwa kwa wajasiriamali4,943 kupitia Asasi ndogo 103. Kati ya waliokopeshwa,wanawake ni 2,040 sawa na asilimia 41 na wanaume ni2,903 sawa na asilimia 59. Kwa wastani, urejeshwaji waMikopo ya Mradi wa SELF umeendelea kuwa wa ufanisi25mzuri katika kiwango cha asilimia 90 hivyo kuwezeshafedha za mkopo kuzunguka na kuwafikia wananchiwengi zaidi.

 • Mheshimiwa Spika, SELF II imetoa mafunzo kwawatendaji280waAsasi115zinaz okopeshawajasiriamali wadogo. Aidha, mafunzo yametolewa kwawajasiriamali wadogo 1,670 katika taaluma yauendeshaji miradi ya biashara. Vile vile, MaofisaUshirika 81 kutoka mikoa ya kanda za Kaskazini naZiwa walipatiwa mafunzo ya utoaji mikopo. Kadhalika,Mradi umeendelea kuelimisha umma kupitia vituo vyatelevisheni vya TBC, ZBC na redio za jamii. Katikamwaka 2014/15, Mradi wa SELF utaendelea namajukumu yake ya kutoa huduma za mikopo kwawajasiriamali wadogo na kuimarisha huduma zakifedha kwa njia ya kujenga uwezo wa Asasizinazokopesha wajasiriamali wadogo.Sheria na Miswada ya Fedha

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya MwanasheriaMkuu wa Serikali ilifanya marekebisho ya Sheriambalimbali za Fedha kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka2013 -The Finance Act, 2013. Lengo la marekebishohayo ni kuweka usimamizi mzuri wa kodi na fedha zaumma. Aidha, Sheria mbalimbali zilizopitishwa naBunge ni pamoja na Sheria ya Mfuko wa Akiba waGEPF wa Mafao ya Wastaafu ya mwaka 2013 -The GEPFRetirement Benefit Fund Act, 2013 na marekebisho yaSheria ya Ushuru wa Bidhaa ya mwaka 2013 (The26Excise (Management and Tariff) (Amendment) Act, 2013)yaliyopitishwa na Bunge katika Mkutano wa 13 mweziDesemba, 2013 yaliyolenga kuondoa kodi ya ushuru wabidhaa kwenye Sim Card.

 • Mheshimiwa Spika, Wizara pia iliandaa Kanunimbalimbali ili kuwezesha usimamizi na utekelezaji waSheria za fedha. Kanuni hizo ni pamoja na Kanuni zaKodi ya Mapato kuhusu Gharama za Kuhamisha -Transfer Pricing Regulations, 2013, Kanuni za Sheria yaUnunuzi wa Umma, 2013 – Public ProcurementRegulations, 2013, Kanuni za Uanzishwaji wa Baraza laUsuluhishi wa Bima, 2013 -The Insurance OmbudsmanRegulation, 2013, Kanuni za Uanzishwaji wa chombocha kushughulikia Rufaa za masuala ya Bima, 2013 -The Insurance Appeals Tribunal Regulations, 2013 naKanuni za Bima Ndogo – The Micro-InsuranceRegulations, 2013.

 • Mheshimiwa Spika, katika mkutano wa Bunge laBajeti unaoendelea Wizara inatarajia kuwasilishaMuswada wa kutunga Sheria mpya ya Kodi yaOngezeko la Thamani – Value Added Tax -VAT na Sheriaya Usimamizi wa Kodi – Tax Administration Act.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizaraitakamilishamaandaliz iyakufanyiamarekebisho Sheria ya Msajili wa Hazina – TreasuryRegistrar Act, Sheria ya Takwimu (Statistics Act) naSheria ya Fedha za Umma -Public Finance Act. Aidha,Wizara ipo katika maandalizi ya kuwezesha kutungwakwa Sheria ya Kodi ya Hoteli -Hotels Tax Act na kufanya27marekebisho ya Sheria ya Mikopo, Misaada naDhamana za Serikali – Government Loans, Grants andGuarantees Act.Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi – PPP

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kupokeana kuchambua maandiko ya miradi inayokusudiwakutekelezwa kwa utaratibu wa ubia kati ya Sekta yaUmma na Sekta Binafsi. Katika mwaka 2013/14,Wizara imepokea na kuchambua miradi minne ya PPP.Katika uchambuzi wa miradi imebainika kwamba kunaupungufu katika upembuzi yakinifu pamoja na ukosefuwa Wataalam wa kufanya upembuzi huo. Aidha, Wizaraimeshiriki kutoa mapendekezo ya kurekebisha Sheriaya Ubia Na. 18 ya mwaka 2010 pamoja na kanuni zakekwa lengo la kuweka usimamizi mzuri wa ubia.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15Wizara imetenga fedha za kuanzisha Mfuko waKuwezesha Utekelezaji wa Miradi ya Ubia -PPPFacilitation Fund.Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramuimepokea na kuchambua taarifa 46 za miamala shukuinayohusu fedha haramu na ufadhili wa ugaidi nataarifa14zakiintelijensia28z imewasilishwa kwenye vyombovinavyosimamiautekelezaj i wa sheria. Aidha, mafunzo ya kudhibitifedha haramu na ufadhili wa ugaidi yametolewa kwawatoa taarifa 135 na washiriki 86 kutoka katikavyombo vinavyosimamia utekelezaji wa Sheria yaUdhibiti wa Fedha Haramu na Mali Athirika. Vile vile,mafunzo hayo yametolewa kwa washiriki 49 kutokaMamlaka za Udhibiti.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramuitatekeleza yafuatayo: kupokea na kuchambua taarifaza miamala shuku inayohusu utakasishaji wa fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi; kutoa mafunzo kwavyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria na kwawatoa taarifa; kutoa miongozo ya kudhibiti fedhaharamu na ufadhili wa ugaidi kwa watoa taarifa;kuratibu zoezi la kutathmini mianya na viashiria vyafedha haramu na ufadhili wa ugaidi katika sektambalimbali nchini; na kuendelea na hatua za kujiungana Umoja wa Kupambana na Biashara ya FedhaHaramu na Ufadhili wa Ugaidi Duniani – EGMONTGroup of Financial Intelligence Units.Tume ya Pamoja ya Fedha

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha imekamilishaStadi ya Kubainisha Mfumo Bora wa Kodi wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, pamoja na kuendelea na29Uchambuzi wa Uhusiano wa Mwenendo wa Uchumi naMapato ya Muungano.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Tume ya Pamoja ya Fedha inatarajiakukamilisha Stadi ya Kubainisha Mwenendo waUchumi na Mapato ya Muungano wa Tanzania, nakufanya Stadi ya Uwekezaji katika Mambo yaMuungano. Aidha, Tume inatarajia kuhuisha Takwimumbalimbali za Stadi zilizofanywa na Tume.Habari, Elimu na Mawasiliano kwa Umma

 • Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kwambaWadau mbalimbali wanapata taarifa zinazohusu kazina majukumu ya Wizara, Wizara imetoa elimu kwaumma kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Aidha,Wizara imeandaa machapisho na vipeperushi kwa ajiliya kuelezea mafanikio, changamoto na njia zilizotumikakatika kukabiliana na changamoto hizo.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara itaendelea kuandaa taarifa kuhusu utekelezajiwa majukumu yake na kuelimisha umma kupitiavyombo vya habari, maonesho, machapisho navipeperushi. Aidha, Wizara itakamilisha Mkakati waMawasiliano.Masuala ya Watumishi

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuchukuahatua mbalimbali za kujenga uwezo wake ili iwezekutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. Hatua hizo ni30pamoja na: kupeleka watumishi katika mafunzo yamuda mfupi na mrefu, kuajiri watumishi 10,kuthibitisha watumishi 21 kazini, kupandisha vyeowatumishi 131, kuboresha mazingira ya kazi kwakukarabati baadhi ya ofisi na kununua vifaa vya ofisi.Aidha, Wizara imeendelea kutoa huduma stahiki kwaWatumishi wa Wizara wanaoishi na virusi vya UKIMWIna kutoa elimu ya afya kwa wafanyakazi.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara inatarajia kuajiri watumishi 257 wa kadambalimbali; kupandisha vyeo watumishi 490; nakuthibitisha kazini watumishi 10. Aidha, Wizarainatarajiakuwapatiawatum ishi642mafunzombalimbali ya kuwajengea uwezo katika kutekelezamajukumu yao, kutoa elimu kuhusu magonjwa sugu nakutoa huduma stahiki kwa watumishi wa wizarawanaoishi na virusi vya UKIMWI.Usimamizi wa Mashirika na Taasisi za Umma

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina imechambuana kutangaza katika Gazeti la Serikali mashirika 10ambayo yanatakiwa kuchangia asilimia 10 ya mapatoghafi katika Mfuko Mkuu wa Serikali. Hadi kufikiaAprili2014,kiasichashil ingibilioni25.0kimekusanywa ikiwa ni asilimia 69.4 ya makadirio yakukusanya shilingi bilioni 36 kwa mwaka 2013/14.31Aidha, katika kutekeleza zoezi la kuingia mikataba yautendaji na Bodi za mashirika ya umma, Wizarainakamilisha majadiliano na Bodi za mashirika yaumma. Vile vile, zoezi la kumpata Msajili wa Hazinalimefikia hatua za mwisho. Matarajio ni kwamba uteuziutafanyika kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara inatarajia kutekeleza yafuatayo: kusimamiautendaji wa Bodi za Wakurugenzi wa mashirika nataasisi za umma na kuingia mikataba ya utendaji naBodi za mashirika ya umma; kusimamia mikakati yakurekebisha mashirika ya umma na kufanya tathminina ufuatiliaji wa Mashirika ya Umma yaliyobinafsishwa;na kuimarisha usimamizi wa mashirika na taasisi zaumma ili kuongeza mapato ya Serikali.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Shirika Hodhi la Mali za Umma (CHC)imeendelea na zoezi la ubinafsishaji na urekebishaji wamashirika ya Umma. Wizara inaendelea na zoezi latathminiyautendajiwamashirik amengineyaliyobinafsishwa kwa lengo la kufahamu kamamakubaliano ya mikataba ya mauzo yanazingatiwa nakuchukua hatua stahiki.Mafao ya Wastaafu na Mirathi

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboreshakumbukumbu za Wastaafu, kulipa mafao na michango32ya kisheria kwa wakati. Hadi Aprili 2014, kumbukumbuza wastaafu 142,014 zimehifadhiwa kwenye mfumo wakompyuta – SAPERION na shilingi bilioni 220.79 sawana asilimia 87 ya makadirio kimelipwa kama mafao yawastaafu wanaolipwa Pensheni na Hazina. Aidha,Wizara imefanya uhakiki wa wastaafu walio kwenyeDaftari la Pensheni la Hazina katika mikoa tisa. Vilevile, shilingi bilioni 522.86 sawa na asilimia 76 yamakadirio ya mwaka kimelipwa kama michango yamwajiri kwa watumishi wa Serikali Kuu na Serikali zaMitaa wanaochangia kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamiipamoja na michango ya Bima ya Afya.

 • Mheshimiwa Spika,Wizaraimeendeleakusimami a na kuratibu shughuli za Mfuko wa Penshenikwa Watumishi wa Umma – PSPF, Mfuko wa Pensheniwa PPF na Mfuko wa Mafao ya Kustaafu – GEPF.Utekelezaji wa Mifuko hiyo kwa mwaka 2013/14ulikuwa kama ifuatavyo:Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma – PSPF

 • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014,Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Ummaulikusanya shilingi bilioni 492.29 ambapo kati ya hizomichango ya wanachama ni shilingi bilioni 402.24 namapato yatokanayo na vitega uchumi ni shilingi bilioni90.05. Aidha, shilingi bilioni 490.95 zilitumika kulipamafao ikiwa ni pamoja na mafao ya kiinua mgongo napensheni za kila mwezi. Katika mwaka 2014/15, Mfukounatarajia kukusanya jumla ya shilingi bilioni 798.12kutoka vyanzo mbalimbali.33Mfuko wa Mafao ya Kustaafu – GEPF

 • Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Mafao ya Kustaafuwa GEPF ambao awali ulikuwa ukijulikana kama Mfukowa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini, umebadili mfumowa malipo ya mafao kutoka akiba na kwenda kwenyemfumo wa pensheni. Mabadiliko haya yamefanywa kwamujibu wa Sheria Na. 8 ya mwaka 2013 iliyopitishwa naBunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. HadiAprili 2014, Mfuko umeweza kusajili jumla yawanachama 10,289 ambapo wanachama 8,138 nikutoka sekta isiyo rasmi. Aidha, michango yawanachama ilifikia kiasi cha shilingi bilioni 31.68 sawana asilimia 79.95 ya lengo la kukusanya jumla yashilingi bilioni 39.62 ifikapo Juni 2014. Vile vile,mapato yatokanayo na vitega uchumi yamefikia shilingibilioni 17.86 ambayo ni sawa na asilimia 84 ya lengo lakukusanya shilingi bilioni 21.26 kufikia Juni 2014.Thamani ya Mfuko hadi mwezi Aprili 2014 imekua nakufikia shilingi bilioni 239.56.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Mfuko utaendelea na jitihada zake za kupanua wigo wawanachama na hivyo kusajili wanachama zaidi katikasekta zote kwa maana ya sekta rasmi na sekta isiyorasmi. Mfuko unatarajia kusajili jumla ya wanachama23,190 na kukusanya michango yenye thamani yashilingi bilioni 47.54. Aidha, mapato yanayotokana navitega uchumi yanatarajiwa kuongezeka hadi kufikiashilingi bilioni 23.99. Thamani ya Mfuko inategemeakukua hadi kufikia shilingi bilioni 310 ifikapo Juni,2015.34Mfuko wa Pensheni wa PPF

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013, Mfukowa Pensheni wa PPF ulikusanya shilingi bilioni 278.57ikiwa ni michango ya wanachama ambayo ni ongezekola asilimia 18 ikilinganishwa na shilingi bilioni 235.89zilizokusanywa mwaka 2012. Aidha, idadi yawanachama wanaochangia katika Mfuko imeongezekakufikia wanachama 247,418 kutoka wanachama203,981 mwaka 2012. Vile vile, mapato yatokanayo nauwekezaji yaliongezeka kufikia shilingi bilioni 305.2kutoka shilingi bilioni 111.15 mwaka 2012 ikiwa niongezeko la asilimia 174.5. Kadhalika, thamani yamfuko imeongezeka kufikia shilingi trilioni 1.49 ikiwa niongezeko la asilimia 36.5 ikilinganishwa na thamani yamfuko ya shilingi trilioni 1.092 ilivyokuwa mwaka 2012.78. MheshimiwaSpika,ThamaniyaMfuko inategemea kukua hadi kufikia shilingi trilioni 1.729ifikapo mwishoni mwa mwaka 2014. Aidha, mapato yauwekezaji yanatarajiwa kufikia shilingi bilioni 180.64.Vile vile, Mfuko unategemea kuandikisha jumla yawanachama 80,000 kutoka katika sekta ya Umma nabinafsi.Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA

 • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2014,mapato halisi ya kodi yalifikia shilingi bilioni 7,771.5sawa na asilimia 75 ya lengo la mwaka la kukusanyashilingi bilioni 10,395.4. Kodi zilizochangia zaidi ni35pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani, Kodi yaKampuni na Kodi ya Mapato ya Ajira ambazo kwapamoja zilichangia zaidi ya asilimia 80 ya mapato hayo.

 • Mheshimiwa Spika, licha ya hatua mbali mbaliambazo zimechukuliwa katika kipindi cha mwaka2013/14, kumekuwa na changamoto katika kufikialengo la makusanyo ya mapato. Sababu zilizochangiakutofikia malengo ni pamoja na: mapato pungufu yaKodi ya Kampuni kuliko ilivyotarajiwa kutoka kwenyebaadhi ya kampuni za madini; kushuka kwamakusanyo hususan Kodi ya Zuio kutokana nakupungua kwa makusanyo kwenye shughuli za utafitiwa gesi na mafuta. Sababu nyingine ni pamoja nakufutwa kwa Tozo ya Kadi za Simu SIMcard levy; namakusanyo hafifu kutoka kwenye Ushuru wa Bidhaawa Huduma za Uhawilisho wa Fedha (Money Transfers).Kwa upande wa Forodha sababu zilizochangiakutofikiwa kwa lengo la makusanyo ni ukuaji mdogo wauingizwaji wa bidhaa kutoka nje, na ongezeko lakuingiza bidhaa kupitia njia zisizo rasmi (panya roads)na bandari bubu.

 • Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kudhibitiukwepaji kodi, wizara kupitia TRA inachukua hatuakadhaa za kudhibiti upotevu wa mapato kupitia bandaribubu na panya roads, kwa kufanya upelelezi ilikuzigundua njia hizo na kuzidhibiti kwa kutumia KikosiKazi cha Kuzuia Magendo (Flexible Anti-SmugglingTeam). Aidha, elimu kwa wafanyabiashara na wananchiwanaozunguka eneo la Pwani imeendelea kutolewa,ushirikiano na vyombo vingine vya udhibiti yaani Polisi36Uhamiaji na Usalama wa Taifa umeanzishwa; nakufanya doria katika maeneo hayo.

 • Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarishamakusanyo ya kodi, Mamlaka inaendelea kuimarishamatumizi ya Mashine za Kieletroniki za kutoa Risiti(Electronic Fiscal Devices-EFDs) ambapo kwa sasainakamilisha zoezi la kuwaingiza wafanyabiashara wotewanaostahili kuanza kutumia mashine hizo, kuanzishaMfumo wa Uthamini wa Mizigo ya Forodha TanzaniaCustoms Integrated System-TANCIS ambao umeanzakutumika mwezi Aprili 2014 pamojamatumizi yamfumo wa kuthamini magari chakavu; na, kuanzishaKitengo cha Kodi ya Kampuni za Kimataifa InternationalTax Unit kwa lengo la kubaini na kudhibiti mianya yakupotea kwa kodi inayolipwa na kampuni za kimataifazilizowekeza nchini.

 • Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka yaMapato Tanzania imeanza kutekeleza makubaliano yaJumuiya ya Afrika Mashariki ya kuweka mazingira yakuanzishwa kwa Mfumo wa Himaya Moja ya Forodha(Single Customs Territory – SCT) kuanzia Januari, 2014.Ili kuhakikisha kwamba mizigo ya nchi jirani haiuzwinchini kinyume na utaratibu wa forodha, mfumo wa ki-eletroniki wa ufuatiliaji wa mizigo inayosafirishwautatumika. Kupitia mfumo huu, mizigo na ama vyombovya usafirishaji hufungwa lakili ya ki-eletroniki(electronic seal) na kifaa cha mawasilaino ambavyohuunganishwa na mfumo mkuu ili kuonesha37mwenendo mzima wa usafiri hadi mzigo husikautakapovuka mpaka wa nchi. Aidha, mbinu nyingine zaudhibiti saidizi kama doria, usuluhishi wa taarifa(reconciliation) na ukaguzi zitatumika ili kuongezaudhibiti.Rufaa za Kodi

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, Bodiya Rufaa za Kodi, imepokea jumla ya rufaa 129 namaombi 37, na imesikiliza na kutolea maamuzi rufaa116 na maombi 28. Aidha, Bodi ipo katika hatua yakuchapisha Ripoti ya Maamuzi yaRufaa za Kodizilizoamuliwa kuanzia mwaka 2009 – 2010. Kwa upandewa Baraza la Rufaa za Kodi, jumla ya rufaa 34 namaombi 4 yamepokelewa ambapo rufaa 41 na maombi9 yamesikilizwa na kutolewa maamuzi. Idadi hiiinajumuisha rufaa na maombi ambayo hayakusikilizwamwaka 2012/13.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Bodi ya Rufaa na Baraza la Rufaa zaKodi itaendelea kupokea, kusikiliza na kutoleamaamuzi rufaa za kodi; kutoa elimu kwa walipa kodijuu ya taratibu za kukata rufaa za kodi; na kutoamafunzo kwa wajumbe wa Bodi na Baraza juu yataratibu za kutatua migogoro ya kodi itokanayo nasheria za Kodi zinazosimamiwa na Mamlaka ya MapatoTanzania. Aidha, Bodi ya Rufaa na Baraza la Rufaa zaKodi linatarajia kuchapisha Ripoti ya Maamuzi ya Rufaa38za Kodi zinazojumuisha maamuzi yaliyotolewa mwaka2011 hadi 2012 kwa ajili ya rejea kwa wadau wake.Huduma za KibenkiBenki Kuu ya Tanzania

 • Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Benki Kuuimeendelea kusimamia Sekta ya Kibenki ambapo katiya kipindi cha Machi 2013 na Machi 2014, idadi yabenki na taasisi za fedha imeongezeka kutoka 51 namatawi 585 hadi 53 na matawi 625 kote nchini. Jumlaya mali ya sekta ya kibenki imekua kutoka shilingitrilioni 17.9 hadi shilingi trilioni 21.1. Kiwango chamitaji kilifikia wastani wa asilimia 18.5 ikilinganishwana kiwango cha asilimia 10 kinachotakiwa kwa mujibuwa sheria. Aidha, Mfumo wa Taarifa za Wakopaji CreditReference Bureau unaendelea vyema, ambapo hadi sasakampuni mbili zimepewa leseni ambazo ni: kampuni yaCreditinfo Tanzania Limited iliyoanza kazi Juni 2013,na kampuni ya Dun & Bradstreet Credit Bureau (T)Limited iliyoanza kazi Septemba 2013. Kampuninyingine kwa jina la Transunion, nayo hivi karibuniimepewa leseni ya muda na inajiandaa kuanza kufanyakazi.

 • Mheshimiwa Spika, Kampuni hizi kwa sasazinaandaataarifazawatejaku tokakwenyekumbukumbu ambazo zinahifadhiwa Benki Kuu.Taarifa hizi bado zinafanyiwa uhakiki kabla ya kuanzakutumika rasmi.Mara baada ya data bank hiyo39kukamilika, makampuni haya ya Credit Referenceyataanza kufanya kazi hiyo kikamilifu na kwa usahihi.Benki Kuu inaendelea kuyahimiza mabenki ambayobado hayajawasilisha taarifa kufanya hivyo.

 • Mheshimiwa Spika, Tarehe 30 Novemba 2013,Marais wa Afrika Mashariki walitia sahihi Itifaki yaUmoja wa Fedha ya Afrika Mashariki. Tukio hili, ndilolimeanzisha safari yetu ya kwenda kwenye hatua yakuwa na sarafu moja ifikapo mwaka 2024. Chini yaItifaki hii, tumekubaliana vigezo ambavyo tutatakiwatufikie kabla ya kuingia kwenye umoja huo na roadmap ya miaka 10 ambayo itaanza kutekelezwa mara tubaada ya nchi zote kuridhia utekelezaji wake. Katikampango huo, mambo muhimu ni; kukamilishautekelezaji wa Umoja wa forodha na Itifaki ya soko lapamoja; kuoanisha mifumo ya kifedh, sera zaubadilishaji wa fedha za kigeni, sera za bajeti, namifumo ya malipo; uhuisha mifumo ya takwimu na;kuhuisha sheria zote zinazohusiana na uanzishwaji waumoja wa kifedhaBenki ya Maendeleo TIB – TIB Development Bank

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14, TIBDevelopment Bank (zamani Benki ya Rasilimali)iliendelea na marekebisho ya ndani ambapo shughuli za40Benki zimegawanywa katika kampuni mbili ambazo niTIB Development Bank Limited inayohusika na shughuliza maendeleo na TIB Corporate Finance Limitedinayohusika na shughuli za biashara.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka ulioishiaDesemba 2013, Benki ya Maendeleo TIB ilipata faida(kabla ya kodi) ya shilingi bilioni 11.9 ikiwa ni ongezekola asilimia 78 toka shilingi bilioni 6.7 zilizopatikanamwaka ulioishia Desemba 2012. Aidha, waraka mizaniawa benki ulifikia shilingi bilioni 408.7 ikilinganishwa nashilingi bilioni 338.4 Desemba 2012;Mikopoiliongezeka kufikia shilingi bilioni 307.0 toka shilingibilioni 242.9 Desemba 2012.

 • Mheshimiwa Spika, Dirisha la Kilimo katika Benkiya Maendeleo TIB liliendelea kutoa mikopo kwawakopaji mbalimbali kwa riba nafuu. Tangu kuanzakwa Dirisha mwaka 2010 hadi kufikia Aprili 2014,maombi yenye thamani ya shilingi bilioni 58.8yaliidhinishwa. Kati ya hizo, shilingi bilioni 33.6zilikopeshwa kwa kampuni za wakulima wadogo na wakati, shilingi bilioni 8.7 zilienda kwa taasisi ndogo zafedha zinazokopesha wakulima wadogo na wa kati; nashilingi bilioni 16.5 zilikopeshwa kwa vikundi vyakuweka na kukopa (SACCOS).Benki ya Maendeleo ya Kilimo – TADB

 • Mheshimiwa Spika, kufuatia uamuzi wa Serikalikuanzisha Benki ya Kilimo, Wizara imetekelezayafuatayo: kuzindua Bodi ya Wakurugenzi wa Benki;41kukamilisha zoezi la upatikanaji wa Mtendaji Mkuu naWakuu wa Idara; kuandaa Muundo wa Benki naMuundo wa Utumishi; kuandaa majukumu yawafanyakazi; kuandaa rasimu ya Mpango wa Biashara;na kupatikana kwa ofisi za Benki. Mwaka 2014/15,Benki ya Maendeleo ya Kilimo inatarajia kupata leseniya biashara, kuajiri wafanyakazi na kuanza kutoahuduma.Twiga Bancorp

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Twiga Bancorp imeendelea kutoa huduma kwa kutumiamatawi makubwa matano na madogo matano. Hadikufikia Aprili 2014, mikopo ya shilingi bilioni 41.9ilitolewa kwa wateja mbalimbali. Uwekezaji kwenyeDhamana za Serikali na Amana katika Benki zingineulikuwa shilingi bilioni 3.6 na mapato yaliyokusanywana Taasisi yalifikia ya shilingi bilioni 3.86.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15Wizara itaendelea kuboresha utendaji wa Taasisi kwakuimarisha uongozi. Aidha, Taasisi itaongeza wigo wahuduma kwa kuanzisha huduma mbalimbali kama vileMax Malipo, Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money nabiashara kwa uwakala. Vile vile, Taasisi inatarajiakufungua tawi jipya Kigamboni.Benki ya Posta – TPB

 • Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wabiashara na kupeleka huduma za kibenki vijijini, Benkiya Posta kupitia ofisi za Shirika la Posta Tanzania42imeziunganisha ofisi nane za Tunduma, Makambako,Peramiho, Masasi, Njombe, Nachingwea, Kilwa naKahama katika mtandao wa TEHAMA na hivyokuongeza idadi ya ofisi za Shirika la Posta ambazozinatoa huduma za kibenki kufikia 17. Aidha, hudumakwa wateja zilitolewa kwa kutumia mashine 185 zaATM.

 • Mheshimiwa Spika, amana za wateja ziliongezekakutoka shilingi bilioni 138.86 mwaka 2012 hadi kufikiashilingi bilioni 170.03 mwaka 2013 sawa na ongezeko laasilimia 22.4. Aidha, uwekezaji katika dhamana zaSerikali uliongezeka kutoka shilingi bilioni 39.67 hadikufikia shilingi bilioni 45.73 katika kipindi hicho sawana ongezeko la asilimia 19.8. Aidha, thamani ya mikopoinayotolewa kwa wateja iliongezeka kutoka shilingibilioni 100.89 hadi kufikia shilingi bilioni 119.73 ikiwani ukuaji wa asilimia 18.7. Vile vile, faida kabla ya kodiimeongezeka kutoka shilingi bilioni 5.67 hadi kufikiashilingi bilioni 6.99 sawa na ongezeko la asilimia 23.4.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014, TPBinatarajia kufikia malengo yafuatayo: kukuza rasilimaliza benki hadi kufikia shilingi bilioni 237.10; kuongezaidadi ya wateja wapya 300,000; kuongeza amana zawateja kufikia shilingi bilioni 200.10; kuongeza mikopoya wateja kufikia shilingi bilioni 47.16; kupata faidakabla ya kodi ya shilingi bilioni 8; na kuendelea nataratibu za kurekebisha sheria iliyoianzisha Benki ilikuisajili chini ya Sheria ya Kampuni.43Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Kifedha

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeanza kufanyamapitio ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Kifedha -National Microfinance Policy, 2000 ili kuondoamapungufu ya kisheria yaliyojitokeza katika utekelezajiwake kwa lengo la kuzingatia mabadiliko ya kiuchumina kijamii pamoja na kuweka mazingira mazuri katikaukuaji wa sekta hiyo. Aidha, katika mwaka 2014/15,Wizara itakamilisha maandalizi ya Sera ya Taifa yaTaasisi Ndogo za Huduma za fedha pamoja na kutungaSheria ya Taasisi ndogo za huduma za kifedha -Microfinance Act.Huduma za BimaMamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima – TIRA

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli zaBima imekamilisha na kutoa Mkakati wa KuendelezaBima ya Watu wa Kipato cha Chini – National MicroInsurance Strategy 2014-2017. Aidha, hadi kufikia Aprili2014, kampuni 30, madalali 100 na mawakala 500 wabima walisajiliwa. Vile vile, mauzo ya bima yaliongezekakutoka shilingi bilioni 406.7 mwaka 2012/13 hadikufikia shilingi bilioni 481.7 sawa na ongezeko laasilimia 18.5.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,TIRA inatarajia kutekeleza yafuatayo: kuendelea namaandalizi ya kufungua ofisi nyingine za kanda;44kuendelea na utaratibu wa uoanishaji sheria na kanuniza soko la bima katika eneo la Afrika Mashariki na lilela nchi za SADC; kuendelea na tafiti za bima ya kilimo,mifugo, pamoja na bima za watu wa kipato cha chini;na kukamilisha taratibu za kuanzisha bima ya Takaful.Shirika la Bima la Taifa – NIC

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara ilikamilisha urekebishaji wa Shirika la Bima laTaifa na usimikaji wa mfumo wa TEHAMA kwa lengo lakuongeza ufanisi. Utendaji wa Shirika kibiasharauliendelea kuimarika ambapo mapato ya bimayaliongezeka kutoka shilingi bilioni 27.38 mwaka 2012,hadi kufikia shilingi bilioni 31.53 mwaka 2013,ongezeko hilo ni sawa na asilimia 15. Mapato hayayalitokana na makusanyo ya bima za mtawanyo, vitegauchumi na mapato mengine.

 • Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Desemba 2013,NIC ililipa madai ya wateja ya shilingi bilioni 8.31.Malipo hayo yalilipwa kwa wateja wa bima za maishakiasi cha shilingi bilioni 5.71 na wateja wa bima zakawaida kiasi cha shilingi bilioni 2.60.

 • Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2014/15,Wizara itaendelea na mkakati wa kuligawa Shirikakatika kampuni mbili, ambayo ni Kampuni ya Bima zaMaisha na Kampuni ya Bima za Kawaida. Aidha,Shirika litaendelea na mkakati wa kujitangaza zaidi na45kuongeza biashara kwa kubuni bima mpya zinazokidhimahitaji ya wananchi.Masoko ya Mitaji na DhamanaMamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Wizara kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji naDhamana imeendelea kusimamia Soko la Hisa la Dar esSalaam, kampuni za udalali na ushauri wa uwekezaji,mipango ya uwekezaji wa pamoja na kampunizilizoorodheshwa kwenye Soko la Hisa . Aidha, Mamlakaimetekeleza yafuatayo: kuzindua Soko la KukuzaKampuni na Ujasiriamali ambapo Benki ya Maendeleoiliorodhesha hisa zake; na kuendelea na maandalizi yauanzishwaji wa soko la Hatifungani za Manispaa.

 • Mheshimiwa Spika, katika kutimiza azma yaSerikali ya kuhakikisha kampuni za Mawasiliano, Gesina Madini zinaorodhesha hisa zake kwenye soko la Hisala Dar es Salaam, Wizara kupitia Mamlaka ya Masokoya Mitaji na Dhamana kwa kushirikiana na wadauiliandaa taratibu zinazotakiwa kuzingatiwa. Aidha,Mamlaka iliendelea kuelimisha umma kuhusu masokoya mitaji na uwekezaji kwa kupitia warsha, matangazokatika vyombo vya habari, vipeperushi na machapisho.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Wizara kupitia Mamlaka ya Masoko ya Mitaji naDhamana imepanga kutekeleza yafuatayo: kukamilishamaandalizi kwa ajili ya uzinduzi wa Soko la Bidhaa;kuzindua mfumo wa uwekezaji kwa kutumia mitandao46ya simu za mikononi (M-akiba) kwa wawekezaji wadogo;kutayarisha taratibu za kisheria na usimamizi wabidhaa na huduma mpya zinazotarajiwa kuingizwasokonizikiwemohatifun ganizahalmashauri;kukamilisha uandaaji wa Mpango Mkuu wa Kitaifa waMaendeleo ya Masoko ya Mitaji na; kuanzisha misingiya kusimamia masoko kwa kuzingatia uzito wa athari.Aidha, Mamlaka itaendelea kuboresha programu yaelimu kwa umma ili kuboresha na kupanua ushiriki wawananchi katika masoko ya mitaji.

 • Mheshimiwa Spika, Serikali iko katika hatua zamwisho za kupata taasisi mbili zitakazoendesha zoezi latathmini ya kupima uwezo wa nchi wa kukopa nakulipa madeni yake. Mwezi Februari 2014, Wizarailiziandikia kampuni za Fitch, Moody’s InvestmentServices na Standard and poors kuwasilisha fomu zaoza mikataba kwa hatua za uchambuzi. Tayari kampuniya Fitch na Moody’s zimewasilisha fomu za mikatabakupitia kwa mshauri mwelekezi Citi Group. Aidha,kuchelewa kwa zoezi hili kulitokana na kampuni hizi zaupimaji (Rating Agencies) kutokukubaliana na aina yafomu za mikataba zinazoandaliwa na serikali pamoja nakuleta nyongeza ya gharama nje ya makubalianoyaliyosainiwa awali.Soko la Hisa Dar es Salaam

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Soko la Hisa Dar es Salaam liliorodhesha Hatifunganiza Serikali zenye thamani ya shilingi bilioni 690 ambazoni asilimia 83 ya makadirio ya mwaka. Kwa upande wahisa za kampuni, Soko liliorodhesha hisa za Benki ya47Maendeleo zenye thamani ya shilingi bilioni 4.5 na hisaza ziada na upendeleo za kampuni ya TOL Gases Ltdzenye thamani ya shilingi bilioni 4.5. Aidha, Kampuniya Swala Oil and Gas (T) Ltd (Australia), MwanzaCommunity Bank ya mkoani Mwanza na UchumiSupermarket(Kenya)ziliwa silishamaombiyakuorodheshwa. Maombi haya yako katika hatuambalimbali za kuidhinishwa.109. MheshimiwaSpika,Thamaniyasokoi meongezeka kutoka shilingi trilioni 14.10 Julai 2013hadi shilingi trilioni 18.06 Aprili 2014, ambayo ni sawana asilimia 28. Mafanikio haya yametokana naongezeko la bei ya hisa za kampuni zilizoorodheshwapamoja na kuorodheshwa kwa kampuni mpya sokoni.Aidha, idadi ya wawekezaji iliongezeka kutoka 180,458mwezi Julai 2013 hadi 192,419 mwezi Aprili 2014.

 • Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha Julai2013 hadi Aprili 2014 hisa zenye thamani ya shilingibilioni 245 ziliuzwa na kununuliwa. Aidha, hatifunganiza Serikali zenye thamani yashilingi bilioni 286ziliuzwa. Kwa ujumla mwenendo wa shughuli za Sokokatika kipindi kilichoishia Aprili 2014 ulikuwa wakuridhisha na viashiria vya mwenendo wa sokovinaonesha mwelekeo chanya.111. MheshimiwaSpika,shughulinyingi nezilizotekelezwa na Soko la Hisa Dar es Salaam nipamoja na: uboreshaji wa Mfumo wa Mnada kwakuweka Mfumo Mpana – Wide Area Network48unaowawezesha madalali kuuza na kununua hisawakiwa mahali popote nchini. Aidha, Soko la Hisa Dares Salaam limekamilisha ukarabati wa jengo la OfisiMbadala Wakati wa Majanga – Disaster Recovery Site najengo hilo limeanza kutumika.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Soko la Hisa Dar es Salaam linatarajia kutekelezayafuatayo: kuendelea kuhamasisha na kuelimishakampuniumuhimuwakuji orodheshaSokoni;kurahisisha shughuli za minada kwa kutumia simu naintaneti; kuboresha mfumo wa kuuza na kununua hisasokoni; na kuendelea na juhudi mbalimbali zinazolengakuongeza ufahamu wa masuala ya masoko ya mitajikwa umma.Dhamana ya Uwekezaji Tanzania – UTT

 • Mheshimiwa Spika, Dhamana ya UwekezajiTanzania imebadilisha muundo wake na kuanzishataasisi ndogo tatu ambazo ni: Taasisi ya Miradi naMaendeleo ya Miundombinu (UTT Project andInfrastructure Development Plc), Taasisi ya UtoajiMikopo (UTT Microfinance Institution – UTT MFI), naTaasisi ya Usimamizi wa Rasilimali za Uwekezaji naHuduma Kwa Wawekezaji (UTT Asset Management andInvestor Services – UTT AMIS). Hadi kufikia Aprili, 2014mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 4.3 imetolewa naUTT MFI kwa wananchi 5,785, wanawake wakiwa 4,744na wanaume 1,041.49

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,UTT MFI inatarajia kuanzisha aina mpya ya mikopo ilikukidhi mahitaji mbalimbali ya wananchi. Mikopo hiyoni: mikopo kwa ajili ya wafanyabiashara nawakandarasi; mikopo kwa ajili ya huduma za afya;mikopo kwa ajili ya kilimo na viwanda vidogo vidogo;mikopo kwa wakala wa huduma za fedha; na mikopo yamatengenezo ya nyumba.

 • Mheshimiwa Spika, UTT AMIS inasimamiamifuko mitano ya uwekezaji wa pamoja ambayo niMfuko wa Umoja, Mfuko wa Wekeza Maisha, Mfuko waWatoto, Mfuko wa Jikimu na Mfuko wa Ukwasi. Katikakipindi cha Julai 2013 hadi Aprili, 2014, thamani yamifuko hiyo iliongezeka kutoka shilingi bilioni 119.03hadi shilingi bilioni 167.37 sawa na ongezeko la asilimia40.62. Ongezeko hili lilitokana na mauzo ya vipandepamoja na ongezeko la thamani za rasilimali zaDhamana ya Uwekezaji. Katika mwaka 2014/15, UTTAMIS imepanga kuanzisha mfuko wa uwekezaji wapamoja katika majumba (Real Estate Investment Trust –REIT).Taasisi za Kitaalam na Huduma NyinginezoOfisi ya Taifa ya Takwimu

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetekeleza yafuatayo:kutayarisha takwimu za mfumuko wa bei kila mwezi;kutayarisha na kusambaza Takwimu za Pato la Taifakwa Robo ya Kwanza na ya pili ya mwaka 2013;50kutayarisha Takwimu za Pato la Taifa kwa mwaka 2013kwa bei za mwaka 2001; na kukamilisha matokeo yaawali ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya BinafsiNchini wa Mwaka 2012. Aidha, Ofisi ya Taifa yaTakwimu imefanya uchambuzi wa taarifa mbalimbali zaSensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na kutoaChapisho la Kwanza la Mgawanyo wa Watu kwa Umrina Jinsia katika Ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya, Kata naShehia; Chapisho la Pili lenye Taarifa za Msingi zaMgawanyo wa Watu Kiumri na Kijinsia. Vile vile,Chapisho la Tatu lenye Taarifa za Msingi zaKidemografia, Kijamii na Kiuchumi kwa Jamhuri yaMuungano wa Tanzania, Tanzania Bara na TanzaniaZanzibar limekamilika.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendelea kuboreshatakwimu rasmi za kiuchumi na kijamii na kutoamachapisho mbalimbali kuhusu Sensa ya Watu naMakazi ya mwaka 2012.Aidha, Ofisi itaendeleakuboresha takwimu za Pato la Taifa kwa kurekebishamwaka wa kizio wa bei za 2001 kwenda 2007 ikiwa nimoja ya hatua za kuboresha takwimu za kiuchumi nakijamii ili zilingane na hali halisi ya maendeleo yauchumi. Vile vile, Ofisi ya Taifa ya Takwimu itaendeleakufanya Utafiti wa Watu Wenye Uwezo wa Kufanya Kaziwa mwaka 2014; Utafiti wa Ajira na Bei wa Mwaka2014; Sensa ya Viwanda ya Mwaka 2014; Utafiti waKilimo wa mwaka 2014/15; na kuendelea namaandalizi ya Sheria mpya ya Takwimu.Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu51

 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2014, Bodi yaTaifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu imeendeshamafunzo ya kitaaluma na kuhudhuriwa na jumla yawashiriki 2,242. Aidha, Bodi imekamilisha silabi mpyaya mitihani ambapo mitihani ya kwanza inatarajiwakufanyika Novemba, 2014. Vile vile, wahitimu 228wamesajiliwakamawatunzavita bu;Wahasibuwahitimu wanaopatiwa uzoefu wa kazi 2,631; WahasibuwaliosajiliwangaziyaCP A1,270;Wahasibuwaliosajiliwa kama Wakaguzi wa Hesabu katika ngaziya CPA-PP 492; Kampuni za Ukaguzi wa Hesabuzilizosajiliwa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguziwa Hesabu 170; na Kampuni za Uhasibu zilizosajiliwana Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu19. Vile vile, Bodi imeendelea na awamu ya pili yaujenzi wa Kituo cha Taaluma ya Uhasibu eneo la Bunju- Dar es Salaam unaotarajiwa kukamilika mwaka2014/15.Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi imesajiliwataalamu 2,404 katika ngazi mbalimbali kwa mujibuwa sheria. Aidha, Bodi imeendesha mafunzo yakitaaluma yaliyolenga kuboresha uwezo wa utendajiunaozingatia maadili. Vile vile, Bodi imetahini jumla yawanafunzi 2,455 ambapo wanafunzi 1,115 walifauluhivyo kufanya idadi ya wahitimu kufikia 24,660. Bodi52pia imeendelea kutoa mafunzo ya vitendo kwa wahitimukutoka vyuo vya elimu ya juu. Katika mwaka 2014/15,Bodi inatarajia kuboresha mazingira ya kujifunzia kwakuboresha mitaala yake ili iendane na soko la ajira laUtandawazi.Bodi ya Michezo ya Kubahatisha

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imeendelea kutekelezamajukumu yake ya kusimamia michezo ya kubahatishaambapo hadi kufikia Aprili 2014, jumla ya kodiiliyokusanywa na Bodi ilifikia shilingi bilioni 10.78 sawana ongezeko la asilimia 14.4. Aidha, Bodi ilichangiashilingi milioni 532.48 katika mfuko mkuu wa Serikalisawa na ongezeko la asilimia 0.85.Taasisi za MafunzoTaasisi ya Uhasibu Arusha

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Taasisi ya Uhasibu Arusha imeendelea kutoa mafunzo53katika fani za uhasibu, ugavi, benki, Usimamizi waFedha, Usimamizi wa Rasilimali, Utawala wa Biashara,Teknolojia ya Habari na Sayansi ya Kompyuta naMasomo ya Kimkakati. Aidha, jumla ya wanafunzi3,341 wamedahiliwa, ambapo kati yao wanaume ni1,847 sawa na asilimia 55 na wanawake 1,494, sawa naasilimia 45.

 • Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana naChuo Kikuu cha Galgotias cha India imeanzishamafunzo ya shahada za uzamili katika sayansi yakompyuta ambazo ni Master in Software Engineering,Master in Information Security na Master in ComputerApplication. Aidha, Taasisi inaendesha E-learningLibrary ambayo imeonesha mafanikio makubwa na piaipo katika hatua za awali za kuanzisha E-learningCenter.

 • Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2014/15,Taasisi inakusudia kuanzisha mafunzo katika: Shahadaya Uzamili ya Ununuzi na Ugavi, Shahada ya MafunzoMkakati -Bachelor in Strategic Studies, Shahada yaSayansi ya Kijeshi – Bachelor in Military Science naStashahada ya uzamili katika mafunzo ya bima -Postgraduate Diploma in Insurance.Chuo cha Usimamizi wa Fedha54

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo cha Usimamizi wa Fedha kilidahili jumla yawanafunzi 9,998 katika fani mbalimbali. Kati ya haowanawake 3,532 sawa na asilimia 35 na wanaume6,466 sawa na asilimia 65. Aidha, Chuo kimeanzishaShahada za Uzamili katika fani za Uhasibu na Fedha,Fedha na Uwekezaji na Rasilimali Watu. Vile vile, Chuokimeanzisha tawi katika Jiji la Mwanza ambapomasomo kwa wanafunzi wa ngazi ya Cheti naStashahada katika fani ya Uhasibu na Benki yalianzakutolewa mwaka 2013.Taasisi ya Uhasibu Tanzania

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Taasisi ya Uhasibu Tanzania ilidahili jumla yawanafunzi 9,769 kati ya hao wanawake 4,776 sawa naasilimia 49 na wanaume 4,993 sawa na asilimia 51Aidha, Taasisi ilianzisha kozi mbili mpya ambazo niUhasibu katika Sekta ya Umma -Public SectorAccounting na Masoko na Uhusiano wa Umma -Markerting and Public Relations katika ngazi za Cheti,Stashahada na Shahada. Vile vile, Taasisi imeanzaujenzi wa jengo la mihadhara katika Kampasi yaMtwara lenye uwezo wa kuchukua wanachuo 500.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Taasisi inatarajia kudahili wanafunzi 9,729, kufunguatawi jipya katika mji wa Kigoma na kuendelea na ujenziwa jengo katika Kampasi ya Mtwara.55Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo kimedahili jumla ya wanafunzi 5,052 kati yaowanawake 2,360 sawa na asilimia 47 na wanaume2,692 sawa na asilimia 53. Aidha, wanafunzi 1,846walihitimu masomo katika kozi mbalimbali ambapo katiya hao wanaume ni 1,037 sawa na asilimia 56 nawanawake walikuwa 809 sawa na asilimia 44. Vile vile,Chuo kimekamilisha ujenzi wa jengo la pili la taaluma.Kadhalika Chuo kimetayarisha taarifa za Hali yaUchumi na Kijamii za Wilaya (District Socio-EconomicProfiles) za Halmashauri za Bunda, Ulanga, Kahama,Geita na Manispaa ya Dodoma.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15,Chuo kitatoa mafunzo ya muda mfupi ya kujenga uwezokwa watendaji namna ya kupanga, kutekeleza nakusimamia mipango ya maendeleo kwenye sehemu zaoza kazi.Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,Chuo kilidahili wanafunzi 269 kati ya hao wanawake108 sawa na asilimia 40 na wanaume 161 sawa naasilimia 60. Aidha, Chuo kimeanzisha Shahada yaUzamili katika Takwimu Rasmi na tayari chuo56kimedahili wanafunzi 32 kutoka nchi za Ethiopia,Ghana, Nigeria, Swaziland na Tanzania.CHANGAMOTO

 • Mheshimiwa Spika,katikakutekelezamajukumu yake, Wizara ilikabiliwa na changamotozifuatazo:i. Kuongeza mapato ya ndani ya Serikali ili kukidhimahitaji yamatumizi ya maendeleo na yakawaida;ii. Mabadiliko ya hali ya uchumi na uongozi katikanchi za washirika wa maendeleo ambapozimepelekea kushindwa kutimizwa kwa baadhi yamiadi;iii. Uwezo wa kusimamia mikataba katika kutekelezabaadhi ya miradi na programu za maendeleo; naiv. Upatikanaji wa mikopo ya kibiashara kwa wakatikunakotokana na kubadilika kwa mashartikutoka kwa wakopeshaji.

 • Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana nachangamoto hizo, Wizara imeendelea kuchukua hatuambalimbali ikiwa ni pamoja na:i. Kubuni vyanzo vipya vya mapato na kudhibitimatumizi pamoja na kupunguza upotevu wamapato;ii. Kuboreshaushirikianonawashirik awamaendeleo yenye lengo la kuwa na uelewa sawakuhusu masuala mbali mbali katika ushirikianowetu;iii. Kuendelea kuzijengea uwezo Wizara, Taasisi naMamlaka za Serikali za Mitaa katika kusimamia57iv.v.na kutekeleza mikataba ya miradi na programu zamaendeleo;Kuendelea kutekeleza Programu ya Maboresho yaUsimamizi wa Fedha za Umma – “Public FinancialManagement Reform Programme (PFMRP)”; naKushauri Wizara, Mikoa na Mamlaka za Serikaliza Mitaa kuzingatia vipaumbele wakati wakupanga na utekelezaji kulingana na bajetiiliyotengwa.Kuanza mazungumzo mapema na wakopeshaji wamikopo ya kibiashara.Mapitio ya Mapato na Matumizi ya Mafungu yaWizara kwa Mwaka 2013/14

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2013/14,majukumu ya Wizara yalitekelezwa katika mafungusaba ya kibajeti. Mafungu hayo ni Fungu 50 – Wizara yaFedha; Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali;Fungu 22 – Deni la Taifa; Fungu 21 – HAZINA; Fungu13 – Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu; Fungu 10– Tume ya Pamoja ya Fedha; na Fungu 7 – Ofisi yaMsajili wa Hazina. Aidha, Fungu 45 – Ofisi ya Taifa yaUkaguzi ambayo inajitegemea linaombewa fedhaBungeni na Waziri wa Fedha kwa mujibu wa Sheria.Fungu 50 – Wizara ya Fedha

 • Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Fungu 50ilitarajia kupata shilingi bilioni 126.48 kutoka vyanzombalimbali vya mapato yasiyo ya kodi ambavyo nimauzo ya mali, uuzaji wa nyaraka za zabuni na mapato58kutoka katika Mashirika ya Umma na Taasisi zaSerikali (Gawio, Michango na Marejesho ya mikopo).Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, makusanyo yalifikiashilingi bilioni 66.79 sawa na asilimia 52.81 ya lengo.Kiwango hicho kinatarajiwa kuongezeka katika robo yanne ya mwaka wa fedha baada ya Mashirika mengikuandaa hesabu za mwaka na ukaguzi wa hesabu hizokukamilishwa.

 • Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 50 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 54.71 kwa ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi bilioni 233.67 kwa ajili ya matumizi yamaendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014, matumiziya kawaida yalifikia shilingi bilioni 36.60 sawa naasilimia 66.89 ya makadirio na matumizi ya maendeleoyalifikia shilingi bilioni 219.97 sawa na asilimia 94.14ya makadirio.Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali

 • Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 23 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 80.83 kwa ajili ya matumizi ya kawaida nashilingi bilioni 4.76 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.Hadi kufikia mwezi Aprili, 2013, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 45.63 sawa na asilimia 56.45 yamakadirio na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingibilioni 1.22.59Fungu 22 – Deni la TaifaMheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi ya Fungu22 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni3,319.01. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014 matumizi yafungu hili yalifikia shilingi bilioni 2,795. 43 sawa naasilimia 84.22 ya makadirio.Fungu 21- HAZINA

 • Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yakawaida ya Fungu 21 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingi bilioni 1,367.29 na matumizi ya maendeleoshilingi bilioni 38.15 . Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014,matumizi ya kawaida yalifikia shilingi bilioni 420.28sawa na asilimia 30.74 ya makadirio, na matumizi yamaendeleo yalifikia shilingi bilioni 19.78 sawa naasilimia 51.85 ya makadirio.Fungu 13 –KitengoHaramuchaUdhibiti waFed ha

 • Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 13 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 1.94 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 0.39 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 0.91 sawa na asilimia 46.90 yamakadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingibilioni 0.07 sawa na asilimia 17.95 ya makadirio.60Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha

 • Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yakawaida kwa Fungu hili yalikuwa shillingi bilioni 2.06,hadi kufikia Aprili, 2014 matumizi yalifikia shilingibilioni 1.04 sawa na asilimia 49.76 ya makadirio.Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina

 • Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 7 kwa mwaka 2013/14 yalikuwa shilingi bilioni38.08 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 1.66 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 33.06 sawa na asilimia 86.8 yamakadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingibilioni 0.62 sawa na asilimia 37.35 ya makadirio.Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

 • Mheshimiwa Spika, makadirio ya matumizi yaFungu 45 kwa mwaka 2013/14 yalikuwashilingibilioni 57.4 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingibilioni 21.45 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Hadikufikia mwezi Aprili, 2014, matumizi ya kawaidayalifikia shilingi bilioni 43.11 sawa na asilimia 75.1 yamakadirio, na matumizi ya maendeleo yalifikia shilingibilioni 2.97 sawa na asilimia 13.84 ya makadirio.61MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWAMWAKA WA FEDHA 2014/15MapatoMheshimiwa Spika, katika mwaka 2014/15, Wizaraya Fedha Fungu 50 inakadiria kukusanya mapatoyasiyo ya kodi yapatayo shilingi126,188,104,000(bilion i 126.19Maombi ya FedhaFungu 50 – Wizara ya Fedha.

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyoa)(b)Matumizi ya kawaida Shilingi 66,239,790,000(bilioni 66.23). Kati ya hizo mishahara ni shilingishilingi5,620,668,000( bilioni5.62)namatumizi mengineyo shilingi 60,619,122,000(bilioni 60.61).Miradi ya Maendeleo Shilingi 29,803,232,000(bilioni 29.71).Kati ya hizoi) Fedha za Ndani – Shilingi 19,350,000,000(bilioni 19.35).(ii) Fedha za Nje – Shilingi 10,453,232,000(bilioni 10.45).Fungu 23 – Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali:62

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyoa)Matumizi ya kawaida – Shilingi 82,170,024,000(bilioni 82.17). Kati ya hizo mishahara shilingi5,012,762,000(bilioni 5.01) na matumizimengineyo shilingi 77,157,262,000 (bilioni77.16).(b)Miradi ya Maendeleo – Shilingi 7,950,000,000(bilioni 7.95) Kati ya hizoi) Fedha za Ndani -Shilingi 4,800,000,000(bilioni 4.80).(ii) Fedha za Nje-Shilingi 3,150,000,000(bilioni 3.15).Fungu 22- Deni la Taifa

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha Shilingi 4,354,865,076,000(bilioni 4,354.86). Kati ya hizo mishahara ni shilingi10,341,136,000 (bilioni 10.34), Deni la Taifa shilingi3,650,612,000,000 (bilioni 3,650.61) na matumizimengineyo ni shilingi 693,911,940,000 (bilioni693.91).Fungu 21 – HAZINA

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyo:63(a)(b)Matumizi ya kawaida Shilingi 790,325,216,000(bilioni 790.32). Kati ya hizo mishahara nishilingi4,015,511,000(bilion i4.01)namatumizi mengineyo shilingi 786,309,705,000(bilioni 786.31) ambazo ni kwa ajili ya matumiziya Idara na Taasisi zilizo chini ya Fungu hili,nyongeza ya mishahara ya Watumishi wa Serikalina matumizi maalum.Miradi ya maendeleo ni shilingi 57,417,015,000(bilioni 57.42). Kati ya hizo;(i)Fedha za Ndani- Shilingi 17,000,000,000(bilioni 17.0)(ii)Fedha za Nje- Shilingi 40,417,015,000(bilioni 40.42)Fungu 13 –KitengoHaramu:chaUdhibit iwaFe dha

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyoa) Matumizi ya kawaida – Shilingi 2,000,000,000(bilioni 2.0).(b) Miradi ya Maendeleo, fedha za nje Shilingi195,000,000 (bilioni 0.19).Fungu 10 – Tume ya Pamoja ya Fedha:

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha Shilingi 2,318,661,000 (bilioni642.32) kwa matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo,shilingi 318,661,000 (bilioni 0.32) ni kwa ajili yamishahara na shilingi 2,000,000,000 (bilioni2.0) nimatumizi mengineyo.Fungu 7 – Ofisi ya Msajili wa Hazina:

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2014/15,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyoa)Matumizi ya kawaida – Shilingi 88,455,278,000(bilioni88.45).K atiyahizoshilingi670,328,000 (bilioni 0.67) ni kwa ajili yamishahara na shilingi 87,784,950,000 (bilioni87.78) ni matumizi mengineyo.(b)Miradi ya Maendeleo – Shilingi 1,943,000,000(bilioni 1.94)Kati ya hizoi)Fedha za Ndani –Shilingi 650,000,000(bilioni 0.65).(ii)Fedha za Nje-Shilingi 1,293,000,000(bilioni 1.29).Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

 • Mheshimiwa Spika, katika fungu hili kwamwakawafedha2013/14,Wizarainaombakuidhinishiwa kiasi cha fedha kama ifuatavyoa) Matumizi ya kawaida shilingi 69,843,825,000(bilioni 69.84). Kati ya hizo mishahara ni shilingi6510,408,402,000 (bilioni 10.41) na matumizimengineyoshilingi59,43 5,423,000(bilioni59.43).(b) Miradi ya maendeleo shilingi 13,011,432,000(bilioni 13.01), kati ya hizoi)Fedha za ndani shilingi 8,000,000,000(bilioni 8.0).(ii) Fedha za nje shilingi 5,011,432,000 (bilioni5.01).HITIMISHO

 • Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zadhati kwa Wakuu wa Idara na Vitengo, Wafanyakazi waWizara ya Fedha wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt.Servacius B. Likwelile na Naibu Makatibu WakuuNdugu Elizabeth J. Nyambibo, Prof. Adolf F. Mkenda naNdugu Doroth S. Mwanyika kwa kazi kubwawanayoifanya katika kutekeleza majukumu ya Wizara.Vile vile, napenda kuwashukuru Wakuu wa Taasisi naWakala wa Serikali chini ya Wizara kwa michango yaokatika utekelezaji wa majukumu ya Wizara.

 • Mheshimiwa Spika, napenda kuwashukuruWaheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza.

 • Hotubahii pia inapatikana katika tovuti ya Wizara(www.mof.go.tz)

  1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

  Tupia Comments