Baraza Kuu la waislamu wa Tanzania (BAKWATA) linawajulisha waislamu na wananchi wote kwa ujumla kuwa Sikukuu ya Eid El-Fitr itakuwa siku ya Alhamisi tarehe /05/2021 au Ijumaa 14/05/2021 kutegemea kuandama kwa mwezi.
Sherehe za Eid El-Fitr kitaifa kwa mwaka huu zitafanyika mkoani Dar es Salaam.Swala ya Eid itaswaliwa katika viwanja vya Mnazi mmoja kuanzia saa 1.30 asubuhi.
Kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania Mh. Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally MBwana anawatakia Waislamu na wananchi wote Sikukuu njema na anawaomba kusherehekea kwa usalama na Amani.