Kutoka Hifadhi ya Taifa Serengeti yalipofanyika Maadhimisho ya Mtoto Njiti Duniani yaliyoandaliwa na Doris Mollel Foundation, Ayo TV inakupa nafasi ya kuona Wadau mbalimbali na Watalii wakitazama Wanyama kutokea angani kwa kutumia Hot Air Balloon.
Tumeongea na Watalii kutoka Mataifa mbalimbali pamoja na Muhudumu wa balloon “Kupanda balloon ni exprience nzuri kwasababu unatazama wanyama kutokea juu tofauti na ile ya kutumia balloon, balloon huruka saa 12 asubuhi kwasababu ya hali ya hewa na mara nyingi hukaa angani kwa saa moja au zaidi”.
Taasisi ya Doris Mollel Foundation leo ikiongozwa na Mkurugenzi wake Doris Mollel imeadhimisha Siku ya Mtoto Njiti Duniani ambayo kwa kawaida huadhimishwa mnamo tarehe 17 Novemba kila mwaka, kwao maadhimisho hayo yamefikia kilele November 20, 2022 ambayo ni Siku ya Mtoto Duniani na yamefanyika Serengeti, Mkoani Mara kwa kugawa vifaa tiba na kufanya utalii katika Hifadhi ya Serengeti ikiwemo kupanda Hot Air balloon na kutalii katika Hifadhi ya Serengeti kwa ajili ya kukuza utalii na kuhamasisha kujitolea.