Dunia nzima itasimama saa chache zijazo wakati ambapo nyota wa soka watakuwa kwenye hatua za mwisho za kinyang’anyiro cha kuwania tuzo ya mwanasoka bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or.
Hafla ya utoaji wa tuzo hizo itafanyika Nyon, Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Geneva, Uswisi ambapo dunia inatarajiwa kumfahamu mchezaji bora wa dunia kwa mwaka 2014 huku wachezaji wanaowania tuzo hiyo wakiwa Cristiano Ronaldo, Manuel Neur na Lionel Messi.
Sambamba na tuzo hiyo ya mchezaji bora wa dunia , makocha watatu bora kwa mwaka 2014 watakuwa wakiwania tuzo ya kocha bora wa mwaka tuzo inayowaniwa na Diego Simeone wa Atletico Madrid, Joachim Loew na Carlo Ancelotti wa Real Madrid.
Ukiachilia mbali tuzo hizo mbili ambazo zinatazamwa sana, nyota wengine kama James Rodriguez, Robin Van Persie na mwanadada Stephanie Roche watakuwa wakikimbizana vikali kwenye tuzo ya goli bora kwa mwaka 2014 .
Katika utoaji wa tuzo hizo kutakuwa na tuzo ya mwanasoka bora wa kike ambayo itakuwa ikiwaniwa na Abby Wambach toka Marekani, Marta wa Brazil pamoja na Nadine Kessler wa Ujerumani.
Nafasi kubwa kwenye tuzo ya mchezaji bora wa dunia inaeleka kwenda kwa Ronaldo ambaye mashabiki wengi wanaamini kuwa atatwaa tuzo yake ya tatu ikiwa ni ya pili mfululizo baada ya kutwaa msimu uliopita.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook