Michezo

Baada ya msimu mbovu Liverpool Balotelli kafunga goli umbali wa mita 27..(+Pichaz&Video)

on

Baada ya kuwa na msimu mbovu katika klabu ya Liverpool uliyopelekea kutoitwa katika timu yake ya taifa ya Italia Mario Balotelli ameanza kurudi katika ubora wake baada ya kufunga moja kati ya magoli mazuri ya faulo katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Udenise.

2CA7444C00000578-3245238-image-a-95_1442952679691

Mario Balotelli alipachika goli hilo dakika ya tano ya mchezo baada ya kupiga faulo kutoka umbali mita 27 na kuingia wavuni moja kwa moja, hili ni goli la kwanza kwa mshambuliaji huyo wa kiitaliano aliyeshindwa kufanya vizuri katika klabu ya Liverpool ya Uingereza na kujiunga kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu yake ya zamani ya AC Milan.

2CA6FF6200000578-3245238-Milan_players_swamp_Balotelli_after_the_24_year_old_gives_his_si-a-47_1442952529386

Balotelli alijiunga na klabu ya AC Milan ya Italia akitokea Liverpool katika dirisha la usajili la mwezi August kwa mkopo wa muda mrefu, Liverpool ililazimika kumtoa kwa mkopo Balotelli baada ya kushindwa kufanya vizuri katika kikosi chao, kwani hadi anaondoka Liverpool Balotelli alicheza mechi 16 na kufunga goli moja pekee.

Video ya goli la Balotelli

https://youtu.be/1eJtmGbLgIQ

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments