Ad
Ad

Top Stories

Mwapachu afariki dunia

on

Waziri wa zamani wa Katiba na Sheria, Bakari Mwapachu amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Andrew Nkuzi ambaye ni msemaji wa familia ya Mwapachu ameeleza kuwa mwili wa mbunge huyo wa zamani utawasili Tanga leo jioni na utahifadhiwa nyumbani kwake Mchukuuni kata ya Tangasisi.

Mwapachu alikuwa Mbunge wa Tanga kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 alipomwachia kijiti Omar Nundu (marehemu) na amewahi kushika nafasi za mbalimbali za  uongozi serikalini katika vipindi tofauti.

MREMBO MDOGO MUUZA SAMAKI, NYANYA ANAINGIZA MAMILIONI “NALIMA MPAKA NALALA SHAMBA, NIMEAJIRI”

Soma na hizi

Tupia Comments