Machafuko mengine Marekani, waandamanaji wameingia mtaani.. wamepora vitu madukani, majengo yamechomwa moto.. bado kisa hiki kinahusishwa na ishu ya ubaguzi wa rangi kwa upande mwingine.
Kijana Freddie Gray alifariki akiwa mikononi mwa Polisi, vurugu zikaanza muda mfupi baada ya kufanyika mazishi yake.
Kifo cha Gray ambaye ni Mmarekani mweusi alifariki siku chache baada ya kulazwa Hospitali akipatiwa matibabu ya majeraha aliyopata kwenye uti wa mgongo baada ya baada ya kupigwa na Polisi.
Watu waliingia mtaani kufanya maandamano ya kupinga kitendo kilichofanywa na Polisi, baadae hali ikabadilika, majengo yakaanza kuchomwa moto na watu wengine wakaanza kuvamia maduka na kufanya uporaji.
Waandamanaji hao walikuwa wakirusha mawe kuyashambulia magari ya Polisi, majengo pamoja na kufanya uharibifu mwingine huku maofisa wa Polisi 15 kujeruhiwa.
Watu 27 wamekamatwa kwa kuhusika na matukio ya uporaji katika maduka ya pombe, dawa na maduka ya kubadilishia fedha pamoja na kuwashambulia maafisa wa Polisi.
Kifo cha Gray kilitokea April 19, hii iishu ni moja ya ambazo zimewahi kusikika zikihusishwa na suala la Polisi wa Marekani kuwaua Wamarekani weusi.. iliwahi kutokea pia Jiji la Ferguson na New York.
Kwa sasa shughuli nyingi Baltimore zimesimama, shule zimefungwa huku vikosi vya zimamoto vikiendelea na jitihada kuzima moto pamoja na Polisi kuwatawanya waandamanaji.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>> twitter Insta Facebook