Michezo

Banda awashinda Manula na Kapombe tuzo ya Emirate

on

Staa wa Simba SC Peter Banda kutokea Malawi amefanikiwa kuibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi March wa Simba SC inayojulikana kwa jina la Emirate Aluminium ACP.

Banda ameshinda tuzo hiyo kwa kuwabwaga golikipa namba moja wa Simba SC Aishi Manula pamoja na mshindi wa tuzo hiyo mwezi uliopita Shomary Kapombe.

Moja kati ya wachezaji wa Simba SC waliofanya vizuri katika mwezi March Peter Banda ni miongoni mwao na alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC kilichotinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuifunga 4-0 USGN kutokea Niger.

Soma na hizi

Tupia Comments