AyoTV

Familia ya marehemu Banza Stone imepata misiba miwili ndani ya dakika 100

on

February 29 2016 misiba miwili imetokea kwenye familia ya marehemu Banza Stone aliyekua mwimbaji hodari wa muziki wa dance Tanzania tokea miaka hiyo, misiba hii miwili imetokea siku 227 toka kutokea kifo cha Banza Stone.

Msiba wa kwanza ni wa Mjukuu wa mama mzazi wa Banza Stone ambapo msemaji wa familia anasema msiba wa pili ni kifo cha Mama mzazi wa Banza, kilichotokea ni kwamba alifariki dakika 60 baada tu ya kifo cha mjukuu wake na inasemekana chanzo ni mshtuko alioupata.

Mjukuu wake alikua anaumwa kifua na alisumbuliwa kwa mwezi mmoja na nusu ambapo wakati wote alikua anaugulia nyumbani na mpaka umauti umemkuta alikua nyumbani ambako aliamua kukaa sababu hakuwa anaumwa sana, hali yake ilibadilika na kuwa mbaya saa kadhaa tu kabla ya kifo.

Khadija Jabir ambaye ndio mama mzazi wa Banza alikuwepo nyumbani baada ya kifo cha mjukuu wake kutokea, aliona kila kitu lakini alionekana kuwa na maumivu makubwa baada ya kifo cha mjukuu wake kipenzi, unaweza kutazama hii video hapa chini kutoka eneo la tukio.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments