Habari za Mastaa

Banza Stone baada ya kuzushiwa kifo, nimemfata nyumbani kwake.

on

.

.

Baada ya kuzushiwa kifo Banza Stone ambaye ni mwimbaji wa longtime kwenye muziki wa dance Tanzania amesema hii sio mara yake ya kwanza kuzushiwa kifo, ni baada ya kuendelea kukaa nyumbani kutokana na kuugua.

Ameongea kwenye Exclusive na millardayo.com na kusema ‘Nilikuwa nasumbuliwa na kinjwa sana na kihoma homa flani kama miezi miwili lakini sasa hivi niko vizuri, naelendelea poa na leo nilienda hospitali daktari akaniambia kuwa nina Malaria’

Kwenye sentensi nyingine Banza amesema ‘Sio mara ya kwanza kuzushiwa kifo, nasikia mara watu oooh banza kafa, mara ooh kila mtu anaongea lake ila mimi niko poa ni mzima naweza kufanya kazi ila kwasasa siko tayari kufanya kazi kwani nitauchosha mwili mwangu

Kuhusu kazi za muziki Banza kasema bado anaendelea >>> ‘Naweza kusema ninaendelea na muziki kama kawaida kwasababu sasa hivi nina kama nyimbo sita  mpya ziko ndani kesho, kesho kutwa naweza nikaamua niachie moja mpaka video ziko tayari sio za bendi bali ni  zangu binafsi’

Unataka kuisikia sauti ya Banza? bonyeza play hapa chini…

Jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>> Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments