Bao la dakika za lala salama la Ousmane Dembele liliipa Paris Saint-Germain (PSG) taji la French Super Cup (Trophee des Champions).
Mabingwa wa Ligue 1 ya Ufaransa msimu uliopita, Parisians waliwafunga mabingwa wa Kombe la Ufaransa Monaco 1-0 kwenye fainali huku bao la mshambuliaji wa Ufaransa likifungwa dakika ya 92 kwenye Uwanja wa Doha’s Stadium 974.
PSG, klabu iliyofanikiwa zaidi katika mashindano hayo, ilitwaa kombe lao la 12.
Mashindano ya mwaka huu yalifanyika katika mji mkuu wa Qatar Doha kwani Ligue 1 ilikuwa imetangaza mwezi Disemba kwamba walitia saini ushirikiano wa taji na Visit Qatar, shirika la kitaifa linalohusika na kuendeleza na kutangaza utalii nchini Qatar.