Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Pichaz za maeneo mengine alikofika Rais Obama kwenye nchi 50 alizotembelea…

on

barack-obama--z

Safari ya Rais Obama ndani ya Kenya imeweka rekodi ambayo sikuwa nafahamu, kumbe kwa kipindi ambacho Rais Obama amekaa madarakani ambacho ni kama miaka saba hivi anakuwa ametembelea jumla ya nchi 50 nje ya Marekani.

President Barack Obama and First Lady Michelle Obama greet the family of Senior Master Sergeant Roland Paramore (not pictured) aboard Air Force One prior to departure en route to New York, Sept. 19, 2011. (Official White House Photo by Pete Souza) This official White House photograph is being made available only for publication by news organizations and/or for personal use printing by the subject(s) of the photograph. The photograph may not be manipulated in any way and may not be used in commercial or political materials, advertisements, emails, products, promotions that in any way suggests approval or endorsement of the President, the First Family, or the White House.

Mmoja ya Wapigapicha wa White House, Pete Souza kazitoa picha 50 ambazo hazikuwahi kuonekana mahali popote !!

Hapa ziko pichaz 12 kati ya hizo mtu wangu.

1-21POQc42jKDN5MMSzHum3g

Aliwahi kufika Msikiti wa Istiqlal uliopo Jakarta, Indonesia… Katikati yuko Imam Ali Mustafa Yaqub, na pembeni mwenye suti na kilemba ni Michelle Obama… November 2010 alikuwa kwenye Msikiti huo na alifuata taratibu za hapo kwa kuvua viatu yeye pamoja na mkewe.

1-ruRy_pbzhKXiEKGMTN3HdA

Kuna wakati alijiachia bila Timu ya Walinzi wake, hii alikuwa anakatisha zake Panama Marekani, April 2015.

1-y2NhcDGt2erm3LkoxP-c2w

Wakati mwingine anaenjoy story na watu wa kawaida kabisa, hapa alikuwa anapiga story na Mkuu wa Wafanyakazi wa Mgahawa wa Esperanza uliopo San Jose del Cabo, Mexico. Hii ilikuwa June 2012.

55b29d4d1d00002f00142981

Hapa alitembelea Sanamu ya Yesu iliyoko Rio De Janeiro, Brazil March 20, 2011.

55b29d4d1d00003000142980

Kwenye safari zake alifika na Egypt pia, akatembelea Mapiramidi ambayo nayo yamo kwenye maajabu ya Duniani.. Hii ilikuwa June 2009.

55b29d4d1400002f002e0b44

Aliwahi fika China pia November 2009. Hapa alikuwa kwenye ukuta mkubwa ambao uko pia kwenye Maajabu ya Dunia, ‘the Great Wall of China’.

55b29d4e1d00002f00142982

Muda mwingine wanakuwa na Stori kwenye mazingira tofauti kabisa na Office, hapa alikuwa na Chancellor wa Ujerumani, Angela Merkel.. Hii ilikuwa Ujerumani June 2015.

55b29d4e1400002e002e0b46

Ishu ya kudance ni kawaida tu kwake, hapa alikuwa na Wanafunzi wa Mumbai, India November 2010.. Pembeni ni mkewe, Michelle Obama.

55b29d4e1400002e002e0b47

November 2010 aliwahi kufika Kamakura, Japan.. Moja ya vitu alivyoenjoy ni kula Ice Cream !!

55b29d4f1400002e002e0b49

Alitembelea pia haya maeneo ya Kihistoria kwenye nchi ya Burma, utamaduni wao inabidi uwe pekupeku bila viatu.. alivua pia, hii ilikuwa November 2012.

55b29d4f1400002f002e0b4a

Hapa ni ndani ya Gereza lililopo Visiwa vya Robben, Cape Town South Africa… Hiki ndio chumba alichowahi kufungwa Hayati Nelson Mandela..  Hii ilikuwa June 2013.

55b29d4f17000026005655dd

Rais Obama alitembelea pia Maeneo ya Makumbusho ya Stonehenge yaliyopo Wiltshire, England… Hii picha imepigwa Sept 2014.

Nitakutumia stori zote ukibonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments