Ad

Top Stories

Baraza la Chuo Kikuu Huria lamtaka Profesa aombe radhi kuhusu waraka wa Corona

on

Baraza la Chuo Kikuu Huria, limekaa kikao cha dharura na kuagiza Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Elifas Tozo Bisanda aombe radhi kwa Wizara ya Elimu, Chuo Kikuu Huria na Umma kwa waraka wa tahadhari ya #CORONAVIRUS alioutoa Februari 8, 2021

Prof. Bisanda alitoa waraka kuwatahadharisha wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho kuhusu ugonjwa wa Corona. Baraza limebaini kuwa yalikuwa maoni binafsi na alikosea kutumia nembo za Serikali

Aidha imedaiwa taarifa ya Prof. Bisanda imeonekana kukinzana na Sera ya Serikali juu ya tahadhari dhidi ya #COVID19 pia haikuwa na takwimu za kuthibitisha uhalali wa baadhi ya taarifa hizo

Baraza limeagiza wanafunzi na wafanyakazi wa chuo waendelee na kazi na masomo kama kawaida. Pia limeomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

BILIONEA AJAYE NI MREMBO MDOGO ANAPATA MAMILIONI SHAMBANI “NAPAMBANA NALALA SHAMBA, NIMEAJIRI”

Soma na hizi

Tupia Comments