Ili kuongeza imani ya wawekezaji, serikali imeanzisha Baraza la Masoko ya Mitaji, ambayo imeundwa kutatua migogoro inayohusiana na shughuli za masoko ya hisa, kanuni za dhamani ya mali, na malalamiko ya wawekezaji, lengo ikiwa na lengo ni kutoa uhakika wa kisheria na kukuza uchumi.
Baraza hilo litakuwa na madaraka kamili katika Mahakama Kuu na itaongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu, akisaidiwa na wajumbe wanne wenye ujuzi katika masoko ya mitaji.
Akizungumza leo katika maonyesho ya wiki ya sheria yanayoendelea jijini Dodoma, Msajili wa Baraza hilo Martin Kolikoli, anasema, “Baraza lina jukumu muhimu katika kufikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050. Kwa kusimamia haki za madai, kuimarisha uwekezaji, na kukuza utawala bora, baraza linaweza kuchangia katika maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”
Anasema baraza hilo linakuja katika wakati ambapo Soko la Hisa la Dar es Salaam limeonyesha utendaji mzuri katika miaka ya hivi karibuni kwa kuongeza bidhaa kwenye soko. Thamani ya kampuni za ndani zilizoorodheshwa iliongezeka kwa asilimia 7.4 ikifikia Sh12.24 trilioni mwaka jana.
“Kwenye maonyesho hayo tutakutana na wadau wetu mbalimbali na kuwaeleza majukumu ya baraza na namna ya kupata haki zao ndani ya masoko ya mitaji,” alisema
Kolikoli aliongeza kuwa baraza litazindua kampeni za elimu ili kuwafahamisha wawekezaji na umma kuhusu masoko ya mitaji na jukumu la baraza hiyo. Aidha, majukwaa ya kidijitali yatakazozinduliwa yatatoa fursa kwa wadau kuwasilisha madai na kufuatilia maendeleo ya kesi.
“Tunaimani kwamba kwa kutekeleza majukumu yetu kama ilivyoainishwa kwenye sheria, tunaweza kulinda haki za wadau kwa kutoa jukwaa la kutafuta fidia kwa makosa, udanganyifu, au ukiukaji wa sheria za dhamani ya mali. Hii itajenga imani miongoni mwa wawekezaji na wadau, kuhakikisha kwamba maslahi yao yanahifadhiwa na kwamba wana njia ya kupata suluhu endapo kutatokea migogoro,” alisema.
Ili kujenga uwezo wake, baraza hiyo kwa sasa inazungumza na taasisi zinazofanana nchini kenya, Zambia, Canada na Afrika Kusini. Ushirikiano huu unalenga kuhakikisha kuwa baraza inafanya kazi kwa ufanisi na inachochea imani miongoni mwa wawekezaji.
Alisema kuwa katika kipindi cha miaka miwili ijayo, inatarajiwa kwamba baraza hii itachangia katika kuongeza uboreshaji wa masoko ya mitaji yenye nguvu zaidi, na kuwa mamlaka inayoongoza kwa rufaa za masoko ya dhamani ya mali za haki na uwazi katika Afrika ya Kusini mwa Jangwa la Sahara, na kukuza imani ya wawekezaji na kudumisha uadilifu wa kifedha.