Michezo

“Barbara alifanya vurugu, akitaka Watoto waingie VVIP” TFF

on

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema limesikitishwa na vitendo vya vurugu vilivyofanywa na baadhi ya Viongozi wa Simba kwenye eneo la kuingilia jukwaa la Watu maalum (VVIP) uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mechi ya Simba SC vs Yanga leo.

Taarifa ya TFF imesema Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez alifika katika eneo hilo akiwa ameongozana na Watoto watatu ambao hawaruhusiwi kuingia katika eneo hilo la VVIP ambapo Watoto hao walikua na kadi zisizo na majina yao kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.

VITUKO VYA SHABIKI WA YANGA FULL MBWEMBWE APIGA GWANDA ZA KIJESHI NA BUNDUKI

Soma na hizi

Tupia Comments