Michezo

Barbara aweka wazi ujio wa mrithi wa Kocha Sven “kesho watamjua kocha mpya” (+video)

on

Uongozi wa Klabu ya Simba umesema kuwa kabla ya mashindano ambayo wameyatambulisha ya Simba Super Cup ambayo yatashirikisha timu tatu hayajaanza watakuwa wameshamtambulisha kocha mpya.

Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba aliondoka Januari 7 muda mfupi baada ya kuifikisha timu hiyo hatua ya makundi kwa ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe.

“Kabla ya mashindano kuanza tutakuwa tumeshamtangaza kocha mpya hivyo kesho mashabiki watamjua kocha mpya wa Simba wasiwe na mashaka, kikubwa ni kwamba tupo imara hatuna mashaka yoyote mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kitakwenda sawa,” Barbara

Soma na hizi

Tupia Comments