Michezo

Barcelona VS Bayern Munich.. zile 3-0 za Messi na Neymar zilipatikana hivi >>Video

on

Mesii & Neymaar

Macho ya fans wa soka duniani ambao wako karibu na ligi kuu ya Mabingwa Ulaya walikuwa wakiicheki hii ya Barcelona VS Bayern Munich.. vichwa vya habari leo michezoni ni ishu ya ushindi wa goli 3-0 walioupata Barcelona.

Lionel Messi alinyoosha mashuti mengi sana kuelekea goli la Bayern lakini hayakuwa na matunda, hakuchoka akaongeza ufundi wake na mpaka dakika 90 zinakamilika alikuwa na jumla ya magoli yake 2.

Messi

Neymar nae akaukamilisha ushindi kwa kufunga goli 1 na kuifanya Barca kutoka kifua mbele.. huenda na wewe una matokeo lakini hukuona magoli yalifungwaje.. hiki kipisi cha video kitakuonesha kila kitu mtu wangu !!

https://www.youtube.com/watch?v=pw3ACwg9maQ

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments