Michezo

Kama hili likitokea usitegemee kuiona klabu ya FC Barcelona ikishiriki Laliga maishani…

on

Rais wa Ligi Kuu Hispania (LALIGA) Javier Tebas na waziri wa michezo wa Hispania  Miguel Cardenal wamethibitisha kama Catalonia ikijitenga na kutoka katika umoja wa Hispania klabu ya FC Barcelona ambayo inatokea Catalonia haitashiriki Ligi Kuu Hispania.

BARCELONA, SPAIN - DECEMBER 22: Catalans hold a large banner reading 'Catalonia is not Spain' as the Catalan anthem played prior to the start of the international friendly match between Catalunya and Argentina at the Camp Nou stadium on December 22, 2009 in Barcelona, Spain. (Photo by Jasper Juinen/Getty Images)

Waziri huyo wa michezo amethibitisha kama Catalonia watajitenga na Hispania basi klabu ya FC Barcelona haitapata fursa ya kushiriki michuano ya soka ya Ulaya. Uchaguzi mkuu wa kikanda wa Catalonia unatarajia kufanyika September 27.

2C9DC17300000578-3243745-image-a-49_1442865045066

Waziri wa michezo wa Hispania Miguel Cardenal

Catalonia wameingia katika mvutano usio rasmi na baadhi ya vyama vya siasa ambavyo vinashawishi Catalonia kujitenga na umoja wa Hispania. Hilo linaweza kutokea kama miongoni mwa vyama hivyo vitashinda viti vingi katika bunge la Catalan.

2C9DC1E000000578-3243745-image-a-48_1442865031155

Rais wa Ligi Kuu Hispania Javier Tebas

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments