Michezo

Barcelona kumfukuza Kocha Mkuu, kama hatotimiza haya

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania sasa itamfukuza kazi kocha wake mkuu Quique Setien mwisho wa msimu 2019/20 endapo Barcelona watamaliza msimu bila Ubingwa wa LaLiga au UEFA Champions League.

Taarifa hizo zinakuja siku chache baada ya FC Barcelona kupoteza point mbili kwa kulazimishwa sare ya 2-2 katika mchezo wao dhidi ya Celta Vigo, kitu ambacho kimewafanya wapinzani wao wakuu wa LaLiga Real Madrid waongoze Ligi kwa tofauti ya point 2.

Hadi sasa FC Barcelona wako nafasi ya pili wakiwa na point 69 wakati Real Madrid wakiongoza Ligi kwa kuwa na point 71 hadi sasa timu zote hizo zimesalia na mechi 6 huku Barcelona wakiwa na changamoto ya geni nyingi ugenini.

VIDEO: AJIB BAADA YA KUSHINDA UBINGWA WAKE WA KWANZA SIMBA “MTANIPIGA MPAKA MNIUE MIMI SIMBA SIHAMI”

Soma na hizi

Tupia Comments