Barcelona wameripotiwa kupiga hatua kubwa kuelekea kumsajili Federico Chiesa kutoka Juventus, lakini bado kuna kazi ya kufanya kabla ya kukamilisha uhamisho huu.
Mwanahabari Adrian Sanchez ameiambia Barca Universal pekee kwamba Barcelona wamefikia makubaliano kimsingi na wakala wa Chiesa, Fali Ramadani Lakini, bado hakuna ofa rasmi kutoka kwa Barcelona kwenda kwa Juventus kwa winga huyo wa Italia.
Chiesa mwenyewe anaonekana kuwa tayari kwa changamoto mpya na mwanzo mpya, na kuhamia Barcelona kunaweza kumpa fursa anayotafuta.
Kwa hali ilivyo, Barcelona wanasawazisha vipaumbele vyao kati ya kukamilisha kuondoka, kusajili wachezaji wapya, na uwezekano wa kumleta Chiesa.
Hii ni kwa sababu klabu hiyo ya Kikatalani kwa sasa inaangazia kuwapakua wachezaji na kumsajili kwa haraka Dani Olmo, usajili wao wa hivi majuzi.
Hivi sasa, kipaumbele kikubwa kwa Barcelona ni kuhakikisha Olmo anasajiliwa rasmi na timu hiyo. Licha ya kusajiliwa mapema Agosti, Olmo bado hajacheza mechi yake ya kwanza kutokana na masuala ya usajili.