Barcelona wanafikiria kutaka kumnunua mchezaji wa zamani Neymar, limeripoti gazeti la Sport la Uhispania.
Jarida hilo linapendekeza kuhama kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 kunaweza kutegemea mustakabali wa Erling Haaland wa Manchester City — huku Neymar akiwa shabaha ya uhamisho ikiwa Barca watamkosa mshambuliaji huyo wa Norway.
Inaripotiwa kuwa wababe hao wa LaLiga wameifanya Haaland kuwa “kipaumbele chao kikuu” kwa msimu wa joto wa 2025 hata hivyo, huku kandarasi ya Neymar Al Hilal ikikamilika msimu ujao wa joto, hivi karibuni ataweza kusaini kwa kilabu anachochagua kwa uhamisho wa bure.
Akiwa na matumaini ya kuchaguliwa katika kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia la FIFA 2026, kurejea Barcelona kunaweza kuwa njia mwafaka kwake kusalia tayari mechi katika miezi kadhaa kabla ya michuano hiyo.
Neymar kwa sasa anajiandaa kurejea uwanjani, akiwa amekaa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja baada ya kupasuka kano yake.