Michezo

Barcelona yamsajili golikipa mpya kumrithi Valdes

on

ter-stegen-bitti-valdes-e-sozlesme-yok-5614713_oKlabu ya FC Barcelona imetangaza kufikia makubaliano na  Borussia Monchengladbach juu ya uhamisho wa golikipa  Marc-Andre ter Stegen kwa ada inayokaribia kiasi cha €9-12 million pamoja na kucheza mechi mbili za kirafiki, gazeti la kihispania la Marca limethibitisha.

Barca walikuwa sokoni kwa muda mrefu wakijaribu kutafuta golikipa baada ya Victor Valdes kutangaza angeondoka kwenye klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu na sasa wamempata mrithi wake Ter Stegen.

Golikipa huyu raia wa Ujerumani atasaini mkataba utakaomuweka Barcelona mpaka 2019.

Tupia Comments