Kijana Barka Seif Mpanda (7) ni miongoni mwa watoto wa kitangazania wanaotazamiwa kufanya makubwa katika soka katika miaka ya baadae.
Dalili hizi zilianza pale clip zake zilipoonekana mitandani na kuanza kuvutia watu mbalimbali ikiwemo club ya Ajax ya Uholanzi ambayo ilivutiwa na kumpa mualiko wa wiki mbili wa kufanya majaribio.
Barka licha ya kuwa ndio mara yake ya kwanza kufika Ulaya kisoka, ilikuwa tofauti na matatajio ya wengi wakiwemo Ajax wenyewe kwa kijana kutoka Afrika na kuwa na uwezo mkubwa.
Uwezo uliwavutia viongozi wa Ajax na kumpa unahodha wa timu ya watoto wenzake, ikiwa ni pamoja na kuonesha uwezo uliyosababisha atwae tuzo mbili za Skills Of The Week na MVP.
Hii Skill Of The Week ni tuzo aliyopewa baada ya kuonekana kufanya vizuri katika ndani ya wiki hususani umahiri wake katika kumiliki mpira na kucheze mpira wakati MVP hii ndio kubwa zaidi kwani ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa ujumla yaani wiki zote mbili za majaribio alionekana mahiri zaidi mbele ya watoto zaidi ya 70 waliyokuwa wamejitokeza.
Barka amewavutia Ajax, kiasi cha Genk kumpa mualiko huku mawakala wa Feyenoord na PSV waliomba kukutana nae, baba mzazi Seif Mpanda bado hajaweka wazi hatma ya mwanae Ajax lakini taarifa zisizo rasmi Barka atajiunga nao, panapo majaliwa pale ambapo itapatikana sababu ambayo haivunji sheria za FIFA za usajili.