Habari za Mastaa

Barnaba kajibu ya jimama aliyetaka kumfungulia duka

on

Leo November 21, 2019 Msanii Barnaba ameamua kufunguka kuhusu taarifa zilizokuwa zikidai ya kwamba kuna mwanamke amejitokeza na kutaka kuwekeza kwenye biashara ya nguo kwa kutumia brand ya Barnaba, huku wawili hao waliwahi kudaiwa kuwa na dalili za mahusiano ya kimapenzi.

Sasa Barnaba amezungumza kuhusu hilo kupitia kipindi cha XXL ya Clouds FM na kutoa ufafanuzi wa hilo kwa kusema haya..>>>“Nafkiri walidhani wanatengeneza brand kwa kum-attack Barnaba lakini sikupenda idea yao ya kuniattack na picha iliyokuja kwenye jamii ni ‘Barnaba anatoka na Jimama na afunguliwa Duka!’ Sikupenda na nikamuonya asitumie jina langu kiholela”

“Kuhusu biashara, Nyie wote mnajua kuhusu mmiliki wa Logo ya Barnaba, nimetengeneza jina langu kwa kitambo sasa, hawezi kutokea mtu akalitumia kirahisi, licha hivyo mimi ninamiliki kampuni ya Hightable Sound ambayo pia niko chini yake. Mimi na huyo Mama tulikuwa kwenye mazungumzo ya kibiashara lakini hatukuweza kufikia muafaka kutokana na hizo janja janja, namuheshimu sana yule Mama.

“Nafkiri walidhani wanatengeneza brand kwa kum-attack Barnaba lakini sikupenda idea yao ya kuniattack na picha iliyokuja kwenye jamii ni ‘Barnaba anatoka na Jimama na afunguliwa Duka!’ Sikupenda na nikamuonya asitumie jina langu kiholela”

“Tulikuwa na uwezo wa kufanya kazi lakini alikosea sana kuihusisha familia yangu, hakuna mtu anayependa kuondoka nyumbani asubuhi akaiacha familia yake haina amani!” – Barnaba

VIDEO: PRODUCER MKENYA AKINUKISHA, ‘UNO’ YA HARMONIZE WATOLEWA YOUTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments