Habari za Mastaa

“BASATA wangeziachia Media, Babu Tale, Mwana Fa msikae kimya” Nay wa Mitego

on

Leo Nay wa Mitego akihojiwa kwenye XXL Clouds FM “Kwa mtazamo wangu nafikiri hiki kilichofanywa na BASATA nafkiri hili lingeachwa kwenye Media kwa sababu kila Media ina Music Department! Hii ni kazi ya Media”.

“Kwenye wimbo wa Mama kwanza nimeambiwa una uchochezi, japo sijaimba Siasa, pili nimeambiwa nimewaimba watu japo kuwa mimi sijataja jina la mtu nimetaja neno Shangazi, tatu nimeambiwa nimeimba Siasa” Nay wa Mitego

“Kwa hiki kinachoendelea kuna muda nawaza kuacha muziki nitafute kazi nyingine ya kufanya! Huu mfumo mpya utawafanya baadhi ya Wasanii washindwe kufanya muziki” Nay wa Mitego

“Mwana Fa usikae kimya, upo Bungeni pia ni Mjumbe wa bodi BASATA, usiwe kama kivuli! Kuna watu kama kina Babu Tale nyie ndio wa kuisemea sanaa, msikae kimya, msiposema mimi nitawasema” Nay wa Mitego

“BILL GATES NA HELA ZAKE ZOTE KAACHWA, MTAACHANA TU, OBAMA NA MKEWE” WATU WA TWITTER

Soma na hizi

Tupia Comments